DAR ES SALAAM.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imepanga kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ili waweze kuzungumzia ongezeko la kodi ya asilimia 10 ya mapato ghafi ya mashirika ambayo imesababisha kupanda kwa gharama za nyumba za Serikali.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imepanga kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ili waweze kuzungumzia ongezeko la kodi ya asilimia 10 ya mapato ghafi ya mashirika ambayo imesababisha kupanda kwa gharama za nyumba za Serikali.
Hata hivyo kamati hiyo inashtukia kodi hiyo sasa ,
wakati Bunge la Bajeti ya mwaka 2013/14 wakiwamo wajumbe wa kamati
walipitisha kodi ya asilimia 10 ya map
ato ghafi kwa mashirika yanayozalisha kwa faida ili kuichangia Serikali.
ato ghafi kwa mashirika yanayozalisha kwa faida ili kuichangia Serikali.
Akizungumza katika kikao kilichoshirikisha
watendaji wa NHC, Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli alisema kuwa
ongezeko hilo ni kubwa, na kwamba limesababisha kuongezeka kwa gharama
za nyumba ambazo wananchi wa kawaida wanashindwa kuzinunua.
“Ongezeko hili limechangia wananchi wa hali ya
chini kushindwa kumudu gharama za nyumba, jambo ambalo linakwenda
kinyume na mkakati wa Serikali wa maisha ni nyumba,”alisema Lembeli.
Aliongeza, kutokana na hali hiyo, viongozi hao
watakaa pamoja na kuangalia namna ambavyo wanaweza kufanya ili waweze
kupunguza gharama hizo, jambo ambalo litakwenda sambamba na mkakati wa
Serikali wa kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya wananchi wasio
na kipato kikubwa.
Akitolea mfano wa nyumba ambayo ilikuwa inauzwa
kwa gharama ya Sh30 milioni, sasa hivi inauzwa kwa gharama ya Sh100
milioni, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa, wananchi wenye kipato
kidogo hawawezi kununua nyumba hizo.
Alibainisha kuwa, kutokana na hali hiyo, Serikali
inapaswa kukaa pamoja na watendaji wake ili kuhakikisha kuwa, kodi hiyo
inaondolewa, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi hao.
Hata hivyo, kamati hiyo imeutaka uongozi wa NHC,
kurudisha hati za nyumba ambazo zilichukuliwa na baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa na kujimilikisha kinyume na taratibu.
“Kuna wafanyabiashara wakubwa wamechukua nyumba
wakati wa utaifishaji, lakini waliambiwa warudishe hizo nyumba wamekataa
kutoa hati,jambo ambalo linakwenda kinyume,”aliongeza.
Alifafanua, kutokana na hali hiyo, kamati hiyo
imewataka watendaji wa shirika hilo kuhakikisha kuwa, nyumba hizo
zinarudi mikononi mwao ili ziweze kutumika kwa manufaa ya wananchi.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Nehemiah
Mchechu alisema kuwa, ikiwa Serikali itapunguza kodi, gharama ya nyumba
inaweza kupungua, jambo ambalo linaweza kuwasaidia wananchi wa kawaida
kuzinunua.
“Tunaiomba Serikali kuangalia upya kodi zilizoongezeka, kwa sababu zimechangia kupanda kwa gharama za nyumba,”alisema Mchechu. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment