BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WASICHANA KUOLEWA NA YEYOTE AU KUZAA NA WANAUME ZA WATU KISA HOFU YA KUZEEKA !!!!.


HIVI sasa watafiti wengi wameonyesha kukubaliana na jambo hilo. Wanasema kwamba, wasichana wengi hubabaika na kufanya mambo yenye kuwaumiza kutokana na hofu kwamba, muda unakwenda haraka na watazeeka. Lakini pia huamini kwamba, starehe zitaisha.

Watafiti hao wanasema, kutokana na maumbile ya wanawake, ambapo miili yao hupevuka haraka, wengi huhofia sana umri. Wameb
aini kwamba, mwanamke anachukia sana kuambiwa amezeeka au hujihami zaidi kuliko mwanaume asionekane kwamba, amezeeka. Kuzeeka kwa wanawake walio wengi kuna maana ya kuchusha na kutokupendwa tena.
Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.

Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu.

Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. 

Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote. Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. 

Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa. CHANZO http://www.jamiiforums.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: