BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU WA THAILAND BI. SHINAWATRA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI TANZANIA.

  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi Waziri mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri mkuu wa Thailand Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa  ameambatana na  mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Kikwete (katikati) . Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake  ya siku 3 nchini Tanzania.  http://michuzijr.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: