a mwili wa mume wake wakati wa misa kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa mazishi, Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako alilazwa. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mwandishi wa kampuni ya IPPMEDIA mkoa wa Morogoro Devotha Minja akiwa mwenye huzuni huku akiwa amemkumbatia Hamida Shariff wa gazeti la Mwananchi Morogoro jana wakati wa kuaga mwili wa bosi wake. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kushoto akimpa pole baba wa Venance George, Mzee George Mhangilwa wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu Venance, Kulia ni Mke wa Marehemu Sauda Mgombelwa.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COMBendera akifafanua jambo huku George Mhangilwa (katikati) na Bonventure Mtalimbo kulia wakisikiza jambo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kusafirisha mwili wa marehemu Venance George kwenda kijiji cha Bukoli Geita kwa ajili ya mazishi. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mtoto wa kiume wa Venance George, Erasto akiwa amekaa katika gari hilo.
Kutoka kushoto mstari wa nyuma, Lilian Justice (Majira) Amina Saidi (Star Tv) na Merina Robert (Mtanzania na Clouds Fm) kila mmoja akiwa ameweka pozi la majonzi wakati wa tukio hilo.
Mwandishi wa Tanzania Daima, Joseph Malembeka kulia akisaidiana na mwenzake kumpa msaada mwanamke ambaye aliishiwa nguvu wakati wa tukio la kuaga.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COMHuyu ndiye Andrew Mpasa ambaye ni Meneja Mauzo gazeti la Mwananchi Morogoro akihakikisha kila jambo lina kwenda sawa katika msiba huo.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU
VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George
Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.
ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule
ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya
msingi.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika
chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.
AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi
wa habari katika kampuni ya,
-Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company
Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport
Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania
Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication
Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo
katika chuo kikuu huria cha Tanzania
ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka
huu 2013.
MWISHO:
-Marehemu alikuwa akisumbuliwa
na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu,
Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe
kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na
watoto wawili wa kike na wa kiume.
SHUKRANI:
-Tunatoa
shukrani zetu za dhati
kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua
mpaka
leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na
marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishia,
Bonveture Mtalimbo.
0 comments:
Post a Comment