Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe
Juma Khamis akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
hali halisi ya moto ulivyoikumba Hoteli ya White Sand iliyoko Kendwa
Nungwi Mkoani humo juzi jioni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set
Bungalows iliyoko katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Abdulsamad Ahmed Said
akikagua athari iliyosababishwa na moto mkubwa uliyoyakumba baadhi ya
majengo ya Hoteli hiyo juzi jioni.
Pembeni
yao aliyevaa kofia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini
“A” Machano Fadhil Machano { Babla } na Nyuma yao aliyevaa suti za
Bahari ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali
Mbarouk.
Baadhi ya Majengo ya Hoteli ya White
Sand iliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Kendwa
Nungwi ikiwa ni miongoni mwa majengo 10 ya hoteli hiyo yaliyoteketea kwa
moto mapaa yake juzi jioni. Picha na Hassan Issa wa OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Hasara
ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja Nukta 2 imepatikana kufuatia kuungua
kwa moto hoteli mbili za Kitalii za White Sand na Sun Set Bungalows
ziliopo katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Wilaya ya Kaskazini “ A” Mkoa wa
Kaskazini Unguja juzi majira ya saa 11.00 za jioni.
Hoteli
ya Sun Set Bungalows inakadiriwa kupata hasara ya zaidi ya shilingi
Milioni mia 400,000,000/- wakati ile ya White Sand iliyoungua zaidi
kutokana na moto huo inakadiriwa hasara ya zaidi ya shilingi Milioni mia
800,000,000/-.
Moto
huo ulisababishwa na hitilafu za umeme katika moja ya majengo ya Hoteli
ya Sun Set Bungalows iliyoezekwa makuti na kutoa cheche za moto
zilizosambaa kwa haraka katika baadhi ya majengo mengine kutokana na
upepo mkali uliokuwa ukivuma katika eneo hilo.
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitokea Bungeni
Mjini Dodoma alifika eneo hilo la tokeo ili kuwafariji Wamiliki,
Wafanyakazi wa Hoteli hizo pamoja na Wananachi wanaozizunguuka Hoteli
hizo kutokana na maafa hayo makubwa kwa uchumi wa Taifa.
Akitoa
ufafanuzi wa mkasa halizi wa tukio hilo Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set
Bungalows Abdullsamad Ahmed Said alimueleza Balozi Seif kwamba Moto huo
umevikumba vyumba Vinane vya kulala wageni, Stoo pamoja na jiko la
kupikia.
Abdullsamad
alisema Wageni wapatao sabini waliokuwemo kwenye vyumba vya Hoteli hiyo
waliweza kuokolewa kwa ushirikiano kati ya Wafanyakazi wa Hoteli hiyo
na Wananchi walioizunguuka Hoteli hiyo jambo ambalo lilileta faraja kwa
Uongozi pamoja na wafanyakazi wake.
Mmiliki
huyo wa Hoteli ya Sun Set Bungalows aliwashukuru wananchi hao, Viongozi
wa Serikali Wilaya na Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na Maafisa wa
Kamisheni ya Utalii kwa msaada wao ulichangia kupunguza machungu ya
janga hilo.
Balozi
Seif Ali Iddi akikagua hali ya tukio la moto huo ambao pia uliathiri
Hoteli nyengine ya jirani ya White Sand ambapo Mmoja miongoni mwa
Viongozi wa Hoteli hiyo Ramadhan Msanif alimfahamisha Balozi Seif
kwamba wakati wakijiandaa kutoa msaada kwa wenzao jirani wa Sun Set
cheche za moto huo pia zikaanza kuvamia Hoteli yao na kulazimika
kukabiliana nalo.
Bwana
Msanif alisema licha ya juhudi walizochukua kukabiliana na moto huo
lakini kasi kubwa ya upepo uliokuwa ukivuma wakati huo ulisababisha
kuathiri mapaa ya nyumba 10 za hoteli hiyo katika kipindi kifupi kwa
vile zilikuwa na mapaa ya makuti.
Akizungumza
na Viongozi, Wafanyakazi wa Hoateli hizo pamoja na Wananchi wa jirani
na Hoteli hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa
wito kwa wananchi kuendelea kusaidia wawekezaji wakati yanapotokea
majanga kwenye maeneo ya vitega uchumi.
Balozi
Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inasisitiza na
kutegemea sekta ya Utalii ambayo kwa sasa inasaidia kuongeza mapato ya
Taifa sambamba na kutoa ajira kwa wananachi wanaovizunguuka vitega
uchumi hivyo.
Hata
Hivyo Balozi Seif aliendelea kuwakumbusha wawekezaji vitega uchumi mbali
mbali Nchini kujenga utamaduni wa kuiwekeza Bima Miradi yao ili wakati
wanapopatwa na majanga au maafa Bima hizo ziweze kuwasaidia.
Alisema
inasikitisha kuona ipo miradi ya kiwango kikubwa cha fedha inayoendelea
kuwekezwa Nchini lakini wamiliki wengi wa miradi hiyo wanashinda
kuikatia bima na hatiame inakufa kabisa pale inapokumbwa na majanga kama
ya moto.
“
Wawekezaji na hata Wafanyabiasharawengi bado wamekuwa wazito kuiwekea
Bima miradi yao na kusahau kwa kuona ghali mpango huo ambao kumbe huwa
unawasaidia wakati wanapopatwa na majanga “. Alifafanua Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi waliopo jirani na
Hoteli hizo kwa juhudi kubwa waliyochukuwa na kusababisha kupungua kwa
hasara kubwa iliyokuwa izikumbe hoteli hizo.
Alisema
juhudi hizo zilizowaongezea nguvu za uokozi wafanyakazi wa hoteli hizo
zimesaidia kuokoa mali na vifaa vya hoteli pamoja na wageni waliokuwa
wakipata huduma ndani ya Hoteli hizo.
“
Nafarajika kusikia kwamba harakati za uokozi wa mali na vifaa katika
Hoteli hizi mbili za White Sand na Sun Set Bungalows za Kendwa hakukuwa
na ripoti za udokozi wa mali kama zilivyotokea Kwenye Hoteli ya Paradise
Beach Resort iliyopo Marumbi wakati ilipowaka moto wiki moja na nusu
iliyopita.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Hoteli hizo kufikiria
kubadilika katika mfumo wa ujenzi wa mapaa ya makuti ili kujilinda na
majanga yanayoweza kuepukwa licha ya kwamba mfumo huo hutoa ajira kwa
wananchi wanaouza makuti yao.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliangalia eneo
lililopembezoni mwa Bara bara mbele ya Skuli ya Msingi na Sekondari ya
Mto Pepo ambalo liko katika hali mbaya kimazingira.
Ziara
hiyo ya ghafla ya Balozi Seif ilikuja kufuatia baadhi ya wananchi
kufanya Biashara katika eneo hilo linalotishia afya za Binaadamu
kutokana na kutuwama kwa maji machafu yanayoweza kusababisha maradhi ya
kuambukiza.
Katika
kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alimuagiza Sheha wa Shehia ya Mto Pepo pamoja na Diwani wa Wadi ya eneo
hilo kufika Ofisini kwake Vuga Jumatatu ya Tarehe 9 Septemba asubuhi
kulijadili suala hilo.
Hali
ya mazingira ya eneo hilo mbali ya kutoa sura mbaya kwa wapita njia na
wageni lakini pia inaweza kusababisha mripuko wa maradhi hasa kwa
wanafunzi wadogo wasiozingatia afya zao wa Skuli ya jirani na eneo
hilo.http://www.zanzinews.com
0 comments:
Post a Comment