AKIWA mmoja kati ya wanadada wanaofanya vizuri sana kwenye Tasnia
ya BongoMovies, Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia
ya kibalozi ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa
Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu.Ana sura na umbo zuri na mvuto mkubwa kutokana na rangi yake nzuri ya ngozi.
Wema Sepetu alizaliwa mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yao yenye watoto wanne wa kike.
Alipata elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini Malaysia kusom
ea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.
Pamoja na filamu hizi Wema ameigiza kwenye filamu nyingine nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa zilizompatia umaarufu na mafanikio makubwa.
Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji wema pia anakipaji kikubwa cha kuimba na pia alishawahi kushiriki mashindano ya urembo na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kujipatia zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4.

0 comments:
Post a Comment