Milioni 5 kwa mwezi zinavyoangamiza
michezo Ilala.
*amri ya rais kikwete yapuuzwa.
*Wadau watishia kufanya maandamano
kuokoa uwanja wa kidongo chekundu.
*Meya adai anayetakaa mazoezi achezee
nyumbani kwake.
WATOTO WAKICHEZA MCHEZO WA SOKA KATIKA UWANJA WA WAZI.
Na Mwandishi wetu,Tanpress.
HIVI ni wananchi wa Ngapi wa Jiji la Dar es Salaam, wanakumbuka Miaka ile ya 90 Jinsi nguli wa sheria Mchungaji Christopher Mtikila alivyovamia uwanja wa Mnazi mmoja na kuvunja uzio.?
Mchungaji Mtikila alifikia hatua hiyo baada ya Manispaa
ya Ilala kumuuzia mwekezaji viwanja vya mnazi mmoja ajenge hoteli lakini kwa
bahati nzuri Mtikila aliibuka kama nabii akaukoa sasa hivi wamerudi tena.
Je wewe ni mdau wa michezo hususani Soka?
Unakumbuka kuwa muda mfupi tu baada ya Rais
Jakaya Kikwete kuanza kazi katika Ikulu ya Magogoni alitangaza
kurejeshwa viwanja vyote vya wazi vilivyokuwa vimeporwa na wajanja wakavigeuza
matumizi ?.
Hakuna takwimu kamili ni viwanja vingapi
vilivyorejeshwa lakini kinachokumbukwa ni ile amri ya Rais aliyosema wazi kuwa
viwanja vya wazi viachwe ili kila anayetaka kucheza acheze…
Rais Jakaya Kikwete akiwa pia mdau muhimu wa michezo alijua umuhimu wa
kuawaacha viwanja hivyo kwa matumizi ya michezo na kizazi kijacho ,lakini leo
miaka mitano baada ya agizo hilo Manspaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,
wamevunja amri hiyo.
Kifupi ni kwamba wametwaa kwa makusudi uwanja
muhimu wa kidongo chekundu uliokuwa unategemewa na wadau wa michezo na kuufanya
kitegauchumi cha watu wachache.
Hivi sasa wamegeuza matumizi ya uwanja huo
kutoka uwanja wa mpira na michezo mingine kuwa soko la magari ya mitumba, gereji
bubu na eneo la kujifunzia magari kwa wanafunzi wanaotaka kuwa madereva.
Kitendo hicho kiliwaudhi wadau wa michezo
wilaya hiyo ambao walifikia hatua ya kutaka kuandamana ili wautwae kwa nguvu
uwanja huo ambao upo kwenye historia ya viwanja vikongwe nchini.
Baada ya taarifa hizo kusambaa jukwaa la habari
kupitia shirika lake la habari nchini (TanPress) liliamua kufanya uchunguzi
kubaini kilichojili nyuma ya kashfa hiyo ambayo inaweza kuleta picha mbaya kuwa
watendaji wa Manspaa ya Ilala wamempuuza Rais wanchi.
Kwanza
Manispaa ya Ilala inaongozwa na Mnec-CCM ,Meya kijana JERRY SILAA ambaye akizungumzia kadhia hiyo
baada ya kuhojiwa na Tanpress alisema kuwa “kwanza ni kuambie ule uwanja tuna maelekezo maalumu kutoka kwa rais
Kikwete”amenukuliwa na Tanpress.
Meya Silaa alipoulizwa kama anakaumbuka amri ya
rais kuwataka viongozi kueheshimu viwanja vya wazi na kwuaachia watoto wacheze,
kwa yeyote anayetaka hivyo kama wameamua kugeuza eneo hilo kuwa maegesho na
soko la magari mabovu alihamaki.
“Sikiliza wewe mwandishi ustake kutuchonganisha
na Rais..ambaye ni mwenyekiti wangu.
Nimesema kuwa tumezungumza naye kabla ya
kubadilisha huo uwanja lakini lazima mjue kuwa sisi ndio mafather City hivyo
masuala ya michezo achana nayo sisi tunatazama miaka 25 ijayo”Meya Silaa
amesema.
Diwani huyo wa kata ya Gongo la Mboto Jimbo la
Ukonga ambaye ni kijana mdogo anayepaswa kulinda na kuetetea viwanja vya
michezo amesema kuwa eneo linalolalamikiwa ni mali ya Manispaa hivyo wanaweza
kulibadili kwa matumizi yoyote wanayoona yanafaaa.
Meya ameuliwa kwamba haoni kuwa akiwa mjumbe wa
NEC-CCM amekwenda kinyume na maagazo ya mwenyekiti wake wa CCM aliyesema
viwanja vya michezo visijengwe ?.
“Aha ha be care fuly nani kwakwambia tumekiuka
utaratibu wa mwenyekiti ...kwanza huwa sifanyi mahojiano na mwandishi bila
kurekodiwa ..nimekuheshimu sana sasa ntakustaki ukinichonganisha na
mheshimiwa.......
“...........Kwanza nani kwakumbia kuwa lile ni
eneo la michezo? Sisi kama wamiliki wake tunajuwa kuwa ni eneo la wazi ambalo
lilikuwa linasubiri kupangiwa shughuli yoyote, sasa tumeona wakati huo bora
tugeuze liwe eneo la kutunzia magari kwa muda wakati huo tunatafuta mwekezaji
ajenge maegesho”anasema.
Hata hivyo baada ya kuulizwa ni wapi
wanamichezo wa ilala watakapokuwa wanatumia kucheza alisema kwa haraka “
wamabie waende Jangwani...ndipo kuna kiwancha cha michezo wanapaswa (kuturoti)
kukimbia hadi jangwani wakifika kule wanakuta miiili inachemka”.
Mstahiki Meya anasema kuwa katika suala la
michezo halina kipaumbele sana katika Manispaa yake kwani sio suala la
maendeleo ‘hatuwezi kuacha kukusanya mapato katika uwanja ule pesa ambayo
ingetumika kutengeneza madawati au kujenga shule tuwachie watu wanacheza
..kachezeni Jangwani ukijaa kila mtu afanyie mazoezi nyumbani kwake............”
Baada ya majibu hayo yenye kukatisha tamaa kwa
wadau wa michezo TanPress iliamua kuzungumza na baadhi ya wadau wa michezo
waliokuwa wanautegemea uwanja huo kwa
shughuli za michezo ambao ni shule ya Sekondari Dar es SALAAM,Gerezani na Shule
ya msingi Gerezani.
Walimu hao wenye dhamana na michezo shuleni kwa
nyakati tofauti wamenukuliwa wakihoji uhalali wa Manispaa ya Ilala kugeuza eneo
hilo matumizi bila kuwashirikisha kwanza huku ikitambua kuwa shule hizo hazina
eneo lingine la michezo.
“Sawa hata kama wakidai kuwa eneo hilo ni la
Manispaa hata sisi shule hizi ni mali ya Manispaa kwa hiyo tuna haki ya
kulalamika ...kwanza hiki ni kipindi cha michezo (UMISETA) huo uwanja
tunauhitaji sana lakini hatuna namna”anasema Mwalimu wa Shule ya Dar es Salaam.
Walimu wa Sekondari hiyo wanasema kuwa shule
yao ambayo inamuunganiko wa shule nyingine ya Gerezani hawakutegemea serikali
kupora uwanja wa shule bila kuwashirikisha na kuwasikia mawazo yao.
Kwa upande mwingine walimu wa shule ya msingi
Gerezani wao kwanza waliogopa kuzungumza na shirika hili ambalo linafanya kazi
ya kukusanya matukio na kusambaza kwenye vyombo vya habari baada ya kuelimishwa
walianza kutoa maoni yao.
Mwalimu kuu wa shule hiyo na Mwalimu wa michezo
walisema walianza kwa kusema kuwa shule yao haina uwanja wa michezo na walikuwa
wakitegemea kiwanja hicho eneo mhimu lakini wameshangaa kukuta kimegeuzwa kuwa
mnada wa magari.
Walimu hao walisema kuwa baada ya kuuliza
kwenye uongozi wa manispaa hiyo waliambiwa kuwa
wakitaka kucheza ,wakacheze kwani uwanja huo ni mkubwa lakini
walipojaribu kuutumia ikashindikana kutokana na kwamba kuna watu wanautumia
kujifunzia magari hivyo wanaweza kugonga watoto.
Wakati hali ikiwa hivyo taarifa kutoka ofisi ya
mahusiano Ilala, zinasema kuwa Mkandarasi aliyetajwa kwa jina la Butiama
Provision Store ndio ilipewa mkataba wa Miezi sita kukusanya ushuru eneo hilo
kwa makubaliano ya kukabidhi shilingi Milioni 5,700,000 kwa mwezi.
Hata hivyo Tanpress iliwasiliana na msemaji wa
Manspaa hiyo Tabu Shaibu ili kupata ufafanuzi zaidi wa sakata hilo ambapo
alisema kuwa ni kweli eneo hilo wameamua kujenga ukuta na kuruhusu magari
yaliyokuwa yanasimama barabara ya Lumumba yaingia ndani ili Manispaa iweze
kujipatia kipato.
Tabu alisema kuwa anashangaa kuona hivi sasa
watu wanaibuka na kulalamaikia uwanja huo wakati ulijadiliwa kwenye kamati za
mipango miji na kama kulikuwa na tatizo maafisa michezo wa manispaa ya Ilala
kwa niaba ya wadau wa michezo wangeweza kutoa ushauri kabla hilo halijafikiwa.
“Hili suala mbona lilijadiliwa kwenye vikao
hadi likapitishwa barazani anayelalamika sasa ni nani mara tunasikia kuna watu
wanapanga kuwandamana ........tumegeuza eneo hilo sehemu ya magari kwa muda
wakati huo tukimtafuta mwekezaji ambaye atakuja kuekeza katika shughuli
zinazofanana na zile za awali ambazo ni michezo”amaenukuliwa Shaibu.
Viongozi wa serikali kubadilisha viwanja
kinyume na utaratibu bila kuwauliza
wananchi tabia hiyo haikuwanza leo kwani hata katika jiji la Mwanza kama sio
wadau kusimama imara tayari Halmashauri ya jiji hilo ilikuwa imeazimia
kubadilisha uwanja mkongwe wa Nyamagana kuwa eneo la ujenzi wa hoteli binafsi.
Hali hiyo ilipigiwa kelele kwa nguvu hadi
viongozi wa Wizara ya ardhi wakaingilia kati na kuun sulu uwanja huo kwa madai
kuwa ni eneo la wazi ambalo linaweza kutumika kuwafadhi wananchi eneo
litataoakea tetemekokubwa au kuzuka moto.
Jijini Dar es Salaam, pia wananchi wake bado
wanakumbukumbu na Manispaa hiyo ya Ilala iliwahi kutaka kumuuzia mwekezaji
uwanja wa Mnazi mmoja ajenge hoteli yake kubwa lakini kwa bahati eneo hilo
liliokolewa na mlinzi wa sheria mchungaji Christopher Mtikila,ambaye alivamia
hapo na kuvunja uzio wa mabati.
je sasa
ni nani atanusulu eneo hilo la kidongo chekundu ambalo licha ya michezo huwa
linatumika katika amikutano ya hadhara, Meya Silaa ametamka kwamba kwasasa
wanatafuta mwekezaji ajenge maegesho ya magari kwa faida ya Manispaa sio watu
wake.
www.mobinday.blogspot.com,
0 comments:
Post a Comment