BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBINU MBADALA NDIYO HII YA RAIS JAKAYA KIKWETE KUTUMIA JESHI KATIKA HARAKATI ZA KUPMBANA NA UJAGILI.


RAIS Jakaya Kikwete amesema ataliamrisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuongoza mapambano dhidi ya ujangili wa tembo na faru na ukataji haramu wa miti kwa shughuli za biashara ambao umefikia kiwango kikub
wa nchini. Amesema sekta ya utalii katika Tanzania imeanza kutishiwa kweli kweli na uuaji wa wanyama hao na biashara haramu ya meno ya tembo na faru.

Kikwete alisema tishio hilo ni kubwa kwa sababu sekta ya utalii inachangia asilimia 17 katika mapato ya taifa na inaajiri watu 300,000. Rais alitangaza uamuzi huo juzi alipozungumza mjini New York, Marekani kwenye mkutano wa viongozi wa nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya wanyama na bidhaa zake pamoja na biashara haramu ya bidhaa za miti na mbao.

Aliuambia mkutano huo ulioandaliwa na Rais Ali Omar Bongo wa Gabon na Serikali ya Ujerumani kwenye Makao Makao ya Umoja wa Mataifa kuwa mwaka 1960, Tanzania ilikuwa na tembo 350,000 lakini kutokana na ujangili idadi hiyo ilishuka hadi 110,000 ilipofika mwaka 2009. Kuhusu faru, Rais Kikwete alisema mwaka 1974 walikuwapo faru 700 katika Tanzania na sasa wako chini ya 100 kwa sababu ya vitendo vya ujangili.

“Katika miaka ya 1980 na 1990 wakati wa kilele cha ujangili katika mikonga ya wanyama, tulilazimika kutumia jeshi kutuliza hali hiyo. “Tuliona matokeo mazuri na tulikuwa na utulivu wa aina fulani. Lakini katika miaka minne iliyopita tumeshuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ujangili kwa ari na kasi mpya.

“Kwa mfano kati ya mwaka 2010 na Julai mwaka, 2013, zaidi ya tembo 1,386 waliuawa katika Tanzania,” alisema na kuongeza:

“Tumechukua hatua kali za kupambana na ujangili ikiwa ni pamoja na sera, sheria na kanuni za kupambana na ujangili. Pia tumetia saini mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kupambana na ujangili huu.

“Vile vile, tumechukua hatua za kukamata majangili na hata kukamata silaha zinazotumika katika ujangili. Kati ya mwaka 2010 hadi katikati ya mwaka huu, 2013 majangili 5,189 wametiwa mbaroni na silaha 1,952 zimekamatwa.

“Isitoshe, vipande vya 3,788 vya meno ya tembo vimekamatwa vikiwa na uzito wa kilo 10,756 zilikamatwa nchini. Nimeamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania kukabiliana na hali hiyo na naamini kuwa tutapata mafanikio makubwa zaidi katika operesheni inayoandaliwa.”

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema bado shughuli za kupambana na ujangili zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mahitaji ya watumishi 4,800 wapya kwa ajili ya kupambana na ujangili hata kama wameajiriwa wafanyakazi 500 tu mwaka huu.

“Ingawa tuna matatizo ya watumishi, bado pia tuna matatizo ya raslimali fedha. Bajeti ya sasa ya dola za Marekani milioni 6.9 kwa ajili ya Idara ya Wanyamapori haitoshi kutimiza yote haya.

“Tunahitaji dola za Marekani milioni 19.4 kwa ajili ya shughuli hiyo na nyongeza ya dola milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi. Tukiachiwa pekee yetu hatuna uwezo. Tunaomba twende pamoja katika hili”. MTANZANIA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: