BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MELI YA MIZIGO YA GOLD STAR ILIYOBEBA SHEHENA TANI 30 YA BANGI YATIWA NGUVUNI.

Meli ya Gold Star iiliyosajiliwa Tanzania ikiwaka moto baada ya mabaharia wake kuichoma iliponaswa ikiwa imebeba dawa za kulevya aina ya bangi katika pwani ya Italia juzi. Picha ya Reuters.

JINA la Tanzania limechafuliwa tena baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamat
wa ikiwa na tani 30 za dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50 milioni (Sh125 bilioni).


Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili kukamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6 bilioni kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.


Habari zilizothibitishwa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Abdi Omar zilisema kwamba meli hiyo ilikamatwa juzi ikiwa na mzigo huo wa bangi.


Alisema baada ya kupokea taarifa za kukamatwa kwa meli hiyo kutoka kwa Polisi wa Kimataifa (Interpol), ofisi yake iliwasiliana na wakala wake aliye na ofisi zake Dubai, Falme za Kiarabu, Kampuni ya Philtex ambayo alisema inafanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya Serikali na kuthibitisha kuisajili.


Alisema meli hiyo ilisajiliwa mwaka 2011 kwa kazi ya kubeba mizigo chini ya Kampuni ya Gold Star.


Alisema kutokana na tukio hilo, Kampuni ya Gold Star imekiuka masharti ya Sheria ya Usajili wa Meli na ile ya Umoja wa Mataifa zinazozuia meli kubeba dawa za kulevya na kuongeza kwamba ofisi yake itafanya uchunguzi na kuchukua hatua.


Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema naye amesikia kupitia kwenye mitandao kwamba hajapata taarifa za kina... “Leo ni Jumapili ni ngumu pia kupata taarifa rasmi kuhusiana na hili.”

“Kesho (leo) tutawasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) ili kufahamu undani wa suala hili. Kuanzia hapo ndipo tutajua nini kinachoendelea, kama waliokamatwa ni Watanzania au la na hiyo bangi waliitoa wapi.”


Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray alisema: “Sina taarifa za tukio hilo, labda tuwasiliane kesho.”


Kama sinema.

Taarifa zilizopatikana jana kwenye mitandao mbalimbali ya kimataifa zinasema meli hiyo ilinaswa maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia waliokuwa Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterania.


Msemaji wa Idara ya Ushuru Italia, alisema: “Meli hiyo ilikamatwa baada ya kupatikana kwa taarifa za kiitelijensia kuwa imebeba dawa hizo, lakini hatukutarajia kama kungekuwa na mzigo mkubwa kiasi hicho na hata wahusika kuipiga moto. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: