VENANCE GEORGE MHANGILWA (40).
Nyumba ya milele ya marehemu Venance
George Mhangilwa aliyefariki dunia Septemba 26 katika hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Morogoro kisha mwili wake kusafirish wa septemba 27 saa 1 usiku kutoka Morogoro kwenda kijiji cha Bukoli Geita na kuzikwa Ivumwa wilaya ya Mbogwe baada ya shughuli ya kuaga mwili kufanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi.
Venance George anayeangalia kamera akiwa na waandishi wenzake wa vyombo mbalimbali vya habari katika mahafali
ya chuo kikuu cha Kiislam Morogoro (MUM) ambapo mahafali hayo Rais
Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi mapema mwaka huu mkoani Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
MOGWE.
MWILI wa Marehemu Venance George (40), umezikwa kijijini kwao Ivumwa wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita huku familia, ndugu na jamaa wakitakiwa kuangalia mustakabali wa watoto walioachwa na marehemu.
Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alilazwa baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu za rambirambi
za Kampuni ya Mwananchi ambako marehemu alikuwa akifanyia kazi, Meneja
wa Idara ya Uhariri, Daniel Mwaijega alisema Venance amemaliza muda wake
hapa duniani kwa kifo chake na kuacha mema ikiwa ni pamoja na familia
yenye watoto waliokuwa wakimtegemea.
Mwaijega alisema ipo mifano mingi ya watoto
kuteseka baada ya mzazi au wazazi wao kufariki na kubainisha kuwa umri
wa watoto wa marehemu ungali mdogo ukihitaji malezi hivyo kuwataka
waombolezaji pamoja na familia kuwalilia watoto.
“Venance nilifanya naye kazi kwa karibu, alikuwa
na bidii kwa kazi na familia, nikiwa hapa nimewaangalia watoto hawa,
ukweli wamenitoa machozi, tusimlilie Venance, bali tuwalilie watoto
hawa,” alisema Mwaijega.
Akizungumza wakati wa kupokea salamu za rambirambi
baba wa George Mhangilwa, alisema kifo cha mwanaye kimemwachia somo la
ushirikiano na kubainisha kwamba ushirikiano aliopewa na rafiki, ndugu
na jamaa wa karibu pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi umekuwa
chachu ya kumuenzi mwanaye kwa kutenda ukarimu. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment