BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NSIIMA CATERING SERVISE MOROGORO YAFANYA KURUFU KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 7 UKUMBI WA MAGADU MESS MOROGORO.

Meneja mauzo wa kampuni ya Nsiima Catering Servise, Jackline Deogratias kushoto akifurahia jambo mara baada ya timu yake kuibuka mshindi dhidi ya Viwawa Kigurunyembe wakati wa tamasha la michezo lililoandal
iwa na kampuni hiyo kuadhimisha miaka saba tangu kuanzishwa kwake kwa michezo mbalimbali katika uwanja wa Magadu mkoani Morogoro. JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Timu ya Nsiima wakikaribia kupata ushidi katika mchezo wa kamba dhidi ya wenzao wa Viwawa ambao Nsiima waliishinda kushinda 2-0.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nsiima Catering Servise kulia, Imaculatha Rutatora na Meneja Mauzo, Jackline Deogratias kushoto wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto cha Mgolole Manispaa ya Morogoro wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wa vyakula, nguo na vifaa vingine vyenye thamani ya sh1.1 milioni ikiwa ni maadhimisho ya miaka saba tangu kuanzishwa kwake mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nsiima Catering Servise Morogoro, Imaculatha Rutatora kushoto akimkabidhi vifaa vya shule mmoja wa watoto mapacha, Dereck na mwenzake Daud Francis (4) kulia kwa niaba ya watoto wenzao wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole baada ya kampuni hiyo kutoa msaada wa vyakula, nguo na vifaa vingine vyenye thamani ya sh1.1 milioni ikiwa ni maadhimisho ya miaka saba tangu kuanzishwa kwake mkoani Morogoro. wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole, Sister Felista Mwinuka na kulia kwake ni Mama Mkuu Msaidizi Sister, Joyce Mmbiki. 
Mchezo wa soka unahitaji maarifa ya ziada kama mchezaji wa Nsiima (9) akimtoka mchezaji wa Viwawa Kigurunyembe ambapo katika mchezo huo Viwawa walikubali kipigo cha bao 1-0 katika uwanja wa Magadu Mess.
Alex Michael akifurahia kukamata kuku jogoo akiwashinda wenzake watatu. JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Timu ya vijana wa Viwawa wakigangamara dhidi ya wapinzani wao Nsiima wakati wa shindano la kuvutana kamba katika tamasha hilo ambapo Viwawa walishindwa kwa kuvutwa 2-0. JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM


Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya kampuni ya Nsiima Catering Servise Morogoro imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Viwawa Kigurunyemba katika mchezo mkali na kusisimua ikiwa ni maadhimisha ya kilele cha miaka saba tangu kuanzisha kwa kampuni hiyo uliofanyika katika uwanja wa Magadu mkoani hapa. 

Bao pekee la Nsiima lilipachika wavuni katika dakika ya 27 kupitia kwa mshambuliaji wao, Godfrey John aliyepiga shuti kali akiwa umbali wa mita 20 baada ya kupokea paso ya Chris Christopher na kumshinda kipa Omega William aliyeruka kuokoa mpira bila mafanikio na kujaa wavuni na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Viwawa Kigurunyembe kutandikwa bao 1-0.

Naye Mkurugenzi hiyo ya kampuni ya Nsiima Catering Servise, Imaculatha Rutatora alisema kuwa maadhimisho hayo yameadhimishwa kwa michezo na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole Manispaa ya Morogoro. 

Rutatora alisema kuwa katika tamasha hilo lilihusisha michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, mbio za magunia na kukimbiza kuku ambapo na kutoa msaada wa watoto yatima wa kituo cha Mgolole mjini hapa.

"Hapa katika ukumbi huu wa Magadu kuna wageni waalikwa zaidi ya 60 ambao nimewaalika ili kujumuika nasi katika maadhimisho haya lengo likiwa ni kufurahia nao pamoja na wanafanyakazi wangu ambapo watapa huduma zote za chakula na vinywaji na maandalizi haya yameghalimu zaidi ya sh1.3Milioni". Alisema Rutatora.

Alitaja washindi wa michezo katika tamasha hilo kuwa ni Viwawa wasichana waliibuka washindi dhidi ya Nsiima ambao walifungwa vikapu 11-3 huku vikapu vya washindi vikitumbukizwa nyavuni na Kamila Lwambano na Magreth Theobal wakati yale ya Nsiima yakifungwa na Mary John na Magreth Charles. 

Katika mbio za kukimbia na magunia Chris Christopher yeye aliibuka mshindi wa kwanza akiwashinda wapinzani wake wanne katika mchezo huo na kukimbiza kuku Alex Michael akifanikiwa kukamata kuku jogoo.

Rutatora alisema katika mchezo wa kuvuta kamba Nsiima waliwatambia Viwawa kwa kuibuka na ushindi wakati wanaume wakiondoka na ushindi wa 2-0 wakati wasichana wenyewe wakiibuka na ushindi wa 2-1.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: