NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kuipikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatas
aray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake Bernabeu.
Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na kutoa mchango wake kunenepesha ushindi.
Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo.
Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat.
Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64, Ronaldo na Benzema.
Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.
0 comments:
Post a Comment