Mkuu wa mkoa
wa Mwanza Evarist Ndikilo akiongoza wanachi kutoa heshima za mwisho kwa
mwili wa Marehemu Askofu wa EAGT Moses, Kulola
Mchungaji
Kadani Limbu ambaye ni Katibu wa Kanisa la EAGT Makao Makuu (Ujenzi)
akisoma wasifu wa marehemu Askofu Kulola aliyezaliwa 1928 katika Kijiji
cha Nyang’honge Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa kupata elimu
ya msingi (Middle School) na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya
mwaka 1946 hadi 1949 kuendelea na masomo na kupata Civil Technician.
Baada
ya kumaliza na kupata utaalamu huo na kuajiliwa kuwa mtumishi wa
serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza kama Mhandisi wa Mchoraji
wa Ramani za majengo na Barabara wakati wa uhai wake aliamua kuacha kazi
na kuanza utumishi wa mungu akifanya kazi kwa kutembea kila mahali
akihubiri Injili kwa watu mbalimbali.
Wasifu
huo ulimwelezea Askofu Kulola wakati wa utumishi wake wa kiroho kuwa
alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia mwaka 1962 akihubiri neno la Mungu
.Baada ya kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na matatizo na
kuwahi kufungwa gerezani na kupigwa na bwana jela na kuumizwa vibaya
muguu wake wa kushoto na kupelekea kupata kilema ambapo aliwekewa mguu
wa bandia.
Marehemu
Askofu Kulola ameacha mke na watoto 10 wajukuu 42 vitukuu 16 na amekuwa
mutumishi wa kiroho tangu akiwa na umri wa miaka 18 ....
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment