BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UTAFITI WA KISAYANSI WAIFANYA TANZANIA KUONGOZA DUNIANI KATIKA ZAO LA KAHAWA.


TANZANIA ndiyo nchi inayoongoza kwa tafiti za kisayansi ambazo zimewezesha kugunduliwa aina mpya 19 za kahawa, imebainika.

Meneja Mipango wa Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa Tanzania (TaCRI), Jeremiah Magesa alisema ugund
uzi huo umeifanya Tanzania kuwa ya juu zaidi katika teknolojia ya kahawa duniani.

Magesa alisema juhudi hizo ndizo zimewezesha TaCRI kupewa kombe na cheti mwaka 2011 kwa ugunduzi wa kahawa bora yenye muonjo wa ladha nzuri zaidi katika ukanda wa Mashariki mwa Afrika.

Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji wa zao la Kahawa TaCRI, Deusdedit Kilambo alisema kwa kawaida dunia ina aiana mbili za kahawa ambazo ni Robusta na Arabika.

Kutokana na tafiti wa zao hili anasema waligundua aina mpya 15 za Arabika nne za Robusta, ambazo alisema zina tija zaidi kwa mkulima kwa kuongeza mazao na hata ubora kwenye soko.

“TaCRI imekuwa ikiendesha programu kabambe kuendeleza aina bora ya kahawa kwa kutafiti ili kupata aina zenye tija zaidi kwa mkulima.” alisema.

Alisema aina zote hizo zina ukinzani dhidi ya magonjwa ambayo yamekuwa hakiathiri uzalishaji wa zao hilo kama vile chulebuni, kutu ya majani na mnyauko fuzari.

Kilambo alisema wakulima wakizingatia kanuni bora za uzalishaji zinazotolewa na TaCRI, kwa kutumia aina hizo 19, Tanzania inaweza kuwa kwenye nafasi ya juu duniani.

Tanzania ni ya 20 kwa uuzaji wa zao la kahawa katika soko la dunia na ni ya tano katika Afrika, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012, zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya zao la Kahawa (ICO).

Brazili inaongoza duniani ikifuatiwa na Vietnam wakati katika Afrika, Ethiopia ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Uganda, Ivory Coast, Papua New Guinea na Tanzania ni ya tano. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: