Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Sadifa Juma
akizungumza katika mkutano wa umoja huo mjini Zanzibar.Wengine ni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi na Katibu Mkuu
wa CCM, Adulrahman Kinana. Picha ya CCM.
DAR ES SALAAM/ZANZIBAR.
MVUTANO mkubwa umeibuka ndani ya Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM), kutokana na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la umoja huo kudhamiria kumng’oa madarakani mwenyekiti wao, Sadifa Juma Khamis.
DAR ES SALAAM/ZANZIBAR.
MVUTANO mkubwa umeibuka ndani ya Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM), kutokana na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la umoja huo kudhamiria kumng’oa madarakani mwenyekiti wao, Sadifa Juma Khamis.
Mgogoro huo ulisababisha kikao cha Baraza Kuu
kilichokuwa kikifanyika Zanzibar juzi, ambacho mgeni rasmi alikuwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapind
uzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi kutofikia mwisho kutokana na baadhi ya wajumbe kumtaka Sadifa na Kamati yake ya Utekelezaji kutoka nje ili wajadiliwe kwa kukiuka kanuni.
uzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Iddi kutofikia mwisho kutokana na baadhi ya wajumbe kumtaka Sadifa na Kamati yake ya Utekelezaji kutoka nje ili wajadiliwe kwa kukiuka kanuni.
Sadifa anadaiwa kukiuka Ibara ya 91 ya toleo la
nane la Kanuni za UVCCM kwa kutangaza uteuzi wa wakuu wa idara tatu za
umoja huo, kabla ya kuundwa kwa Kamati ya Utekelezaji ambayo kimsingi
alipaswa kushirikiana nayo kuwateua, kabla ya kuidhinishwa na baraza
kuu.
Habari kutoka katika mkutano huo uliofanyika
katika Ofisi ya CCM, Kisiwandui zinasema Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana ndiye aliyeokoa jahazi baada ya kuingilia kati mvutano baina ya
baadhi ya wajumbe na Sadifa.
Inaelezwa pia kuwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM,
Sixtus Mapunda naye alionja chungu ya mgogoro huo pale alipopingwa
vikali na wajumbe, alipojaribu kumtetea mwenyekiti wake.
Hata hivyo, Sadifa na Mapunda kwa nyakati tofauti
jana walisema kuwa mkutano huo ulimalizika bila tatizo na ulikuwa na
ajenda moja tu ya kumthibitisha Katibu Mkuu jambo ambalo lilifanyika
kama ilivyokuwa imepangwa.
“Kwa mujibu wa kanuni, mwenyekiti ndiye mwenye
mamlaka ya kufungua na kufunga kikao na vyote hivyo tulifanya, hakuna
kikao kilichovunjika,” alisema Sadifa.
Alipotakiwa kueleza kuhusu kanuni anayodaiwa
kuivunja, alikataa kuzungumzia suala hilo akitaka kwanza mwandishi
amwambie chanzo chake cha habari.
“Nani huyo aliyetaka nitoke, wewe nisikilize, kuna
watu ambao wanajua kabisa unataka kuzungumza nini hata kabla hujasema
na mmoja wa watu hao ni Sadifa kwa hiyo nilishajua kabisa ni nini
unataka,” alisema Sadifa na baada mwandishi kuendelea kumuuliza maswali
alikata simu.
Kwa upande wake, Mapunda alisema: “Mkutano
ulifanyika na kumalizika kama ulivyokuwa umepangwa. Ule ulikuwa ni
mkutano maalumu na ulikuwa na ajenda moja tu, mwenyekiti aliufungua na
kuufunga kama ilivyokuwa imepangwa. Ajenda ilikuwa ni kunithibitisha
mimi tu (kuwa katibu wa UVCCM) na baada ya hilo kufanyika nilikaribishwa
na mimi nikazungumza na nikamaliza”. MWANANCH.
0 comments:
Post a Comment