BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAHAMIAJI HARAMU 863 RAIA WA MALAWI WAJISARIMISHWA KATIKA OFISI KUU ZA UHAMIAJI JIJINI DAR ES SALAAM.


PICHA YA MAKTABA: JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM NOVEMBA 03, 2011.
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro akiwa anawalinda raia wa Ethiopia 103 baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi mkoa huo wakati wakisubiri kusomewa shikataka la kuingia nchini kinyume na sheria baada ya kukamatwa katika mji mdogo wa Mikese barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro mkoani hapa.

WAHAMIAJI haramu 863 raia wa Malawi wamejisalimisha katika Ofisi za Uhamiaji makao makuu Dar es Salaam jana. Kujisalimisha kwa wahamiaji hao kumeongeza idadi ya wahamiaji haramu kutoka nchi hiyo kufikia 1,893. 


Ofisa uhamiaji wa mkoa huo Grace Hokororo, aliliambia MTANZANIA jana kuwa idadi kubwa ya wahamiaji hao wamebainika kuwa na kadi za kupiga kura.

“Leo tu (jana) wahamiaji 863 raia wa Malawi wamejisalimisha ofisi za uhamiaji.

“Katika mahojiano nao wengi wana kadi za kupigia kura, idara ya uhamiaji hatuziamini kadi hizo tunachohitaji ni uthibitisho wa uraia.

“Idadi hii ni kubwa inaonyesha jinsi ambavyo wahamiaji haramu kutoka Malawi walivyo wengi b nchini.

“Tunapinga kabisa tuhuma zinazoelekezwa kwa Serikali kuwa inaendesha operesheni hii kwa ajili ya Wamalawi tu,” alisema.

Hokororo alisema baada ya kujisalimisha kwa wahamiaji hao hatua inayofuata ni kuwatambua.

Baada ya kuwatambua mpango utakaofuata ni pamoja na kuwarejesha makwao.

Katika hatua nyingine wahamiaji haramu 25, raia wa Burundi wamekataa kurejeshwa makwao baada ya kudai kuwa wao ni raia halali wa Tanzania.

“Wahamiaji wengi hawatoi ushirikiano, wengine ni waongo wanadai wamezaliwa Tanzania tunapowafuatilia tunabaini kuwa walizaliwa miaka ya 1980 wakati wanadai kuwa walizaliwa kabla ya miaka hiyo,”alisema Hokororo.

Ofisa huyo alisema kutokana na changamoto hiyo idara ya uhamiaji ina mpango wa kuwafuatilia kwa undani kubaini ukweli.

“Wakati tunaendelea na msako hu, tunajipanga kwenda mikoani ambako wahamiaji wanadai kuwa walizaliwa huko.

“Zipo changamoto mbalimbali zikiwamo uhaba wa maofisa wa uhamiaji ila hazitakwamisha operesheni hii.

“Timu yetu inajipanga kufika vijijini kupata ushahidi wa hawa wahamiaji 25 na wengine ambao watadai kuwa ni Watanzania.

“Kama watasema wanatoka Kigoma tutaenda Kigoma hadi vijijini mpaka kwenye shule walikosoma na hospitali walikozaliwa,”alieleza ofisa huyo.

Hokororo alisema kuna taarifa kuwa baadhi ya wahamiaji haramu wameajiriwa katika taasisi mbalimbali zikiwamo za Serikali.

“Zipo taarifa kuna watu wana hati za kusafiria na vyeti vya kuzaliwa, wengine wameajiriwa katika taasisi mbalimbali, tunafuatilia hizi taarifa tunaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi,”alisema.

Hivi karibuni idara ya uhamiaji iliwakamata raia saba wa Nigeria akiwamo Mchungaji wa Kanisa la Kimataifa la Life Changer Chapel, lililopo Sinza ‘E’ aitwaye Grace Dangana Omotok.

Mchungaji huyo alikiuka mashariti ya kibali chake ambacho hakimruhusu kumuingiza raia yeyote nchini.

Msako wa wahamiaji haramu unatekelezwa kufuatia agizo la Rais Kikwete alilolitoa Julai 26, mwaka huu mkoani Kagera, ambapo aliwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini kwa hiari yao. MTANZANIA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: