BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAMGAMBO WA AL-SHABAAB TISA WAPIGWA RISASI NA VIKOSI VYA USALAMA VYA KENYA NI BAADA YA KUVAMIA JUMBA LA MADUKA YA KIFAHALI LA WESTGATE SIKU YA JUMAMOSI NA KUUA RAIA ZAIDI 60 NA MAJERUHI 175 MJINI NAIROBI.

Watu wakitafuta usalama wao wakati wanejeshi walipoingia kwenye maduka ya kifahari ya westgate kufanya operesheni.
VIKOSI vya usalama nchini Kenya vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima la Westgate. 

Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa

Duru kutoka shirika la AFP zinasema kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.

Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.

Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.

Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.

Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.

Karibu wanajeshi kumi na wawili wako kwenye paa la jengo la Westgate wakishika. Anauliza je shughuli ya kuwasaka magaidi imekamilika ?.

Saa 11:15 jioni Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wananchi walioyaacha magari yao katika jengo hilo wametakiwa na maafisa wa usalama kwenda kuyachukua, ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa

Saa 11:14 jioni Milio ya risasi ilisikika mchana huu huku majeshi ya Kenya yakiendelea kukabiliana na magaidi waliosalia ndani ya jengo la Westgate. Mapema serilali ilisema kuwa magaidi sita waliuawa usiku wa kumkia leo na wengine hapo jana. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: