TAASI za kiraia Zanzibar zimesema hazijawahi kushirikishwa katika kuiboresha Muswada wa sheria ya Mabad
iliko ya Katiba Mpya Tanzania.
Taasisi hizo saba ambazo zinaongozwa na Baraza la
Katiba Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Pr. Abdul Sharif zilisema Bunge
halijawatendea haki kwa kunyimwa fursa ya kutoa maoni katika sheria
hiyo. Waliyasema hayo huko Bwawani Zanzibar walipokuwa wakizungumza na
waandishi wa habari jana.
Katibu wa Zanzibar Youth Forum Alimasi Mohammed
Ali alisema kushirikishwa Serikali ya Mapinduzi haina maana kwamba na
wananchi wameshirikishwa.
“Muswada ule ulipokuja mwanzo, viongozi wa
serikali waliitwa Bwawani na sisi raia wa kawaida tuliitwa katika skuli
ya Haile Salasi kutoa maoni yetu” alisema Ali.
Alisema haoni sababu kwa muswada huu wa sheria
hiyo kupewa fursa serikali peke yake na wao kama raia wakaonekana kama
hawana maana.
“Walijua fika kwamba Wazanzibar hawawezi kukubali kuwa wachache katika Bunge la Katiba na bara kuwa wengi” alisema Ali.
Alifananisha na tume ya mabadiliko ya katiba
kwamba ilikwenda kwa wananchi mara mbili tofauti. Kwa nini kamati ya
Katiba na Sheria ishindwe. “Hatukubaliani hata siku moja kwa Bara wawe
na 64% na Zanzibar kubakia na 36% wakati ni nchi mbili sawa katika
Muungano” alieleza Ali.
Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar Pr Abdul
Sharif alisema kwa mujibu wa sheria ingalikuwa vyema Muswada huo
ukaonekana katika magazeti ili wananchi watoe maoni yao.
“Mimi mwenyewe nilikuwa na mapendekezo yangu lakini hawakunipatia fursa ya kutoa mawazo yangu” alisema Pr. Sharif.
Alisema wameutoa mswada huo katika kabati na
kuupeleka Bungeni tu, halafu wanajidai wananchi wamepata fursa si kweli.
Aliendeleaa.
Taasisi ambazo zimeshiriki mkutano huo ni pamoja
na TAMWA, Zanzibar Youth Forum, Zanzibar Law Society, Baraza la Katiba,
Pemba Press Club, Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar
na ZAFELA. MWANANCHI.
1 comments:
kitaeleweka tu.
Post a Comment