BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IGP MSTAAFU OMARI MAHITA AKANUSHA UVUMI WA YEYE KUPOOZA MKOANI MOROGORO.



 
Mkuu wa jeshi la polisi mstaafu nchini, Omari Mahita akiwa nyumbani kwake Forest mkoani Morogoro akiwa mweenye afya tele ambapo mwandishi mpiga picha alimwomba apate picha wakati kiongozi huyo akionyesha ukakamavu kama picha inavyoosha.

Na Lilian Lucas,Morogoro.
UVUMI uliozagaa juu ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi mstaafu Omary Mahita kuwa ni mgonjwa na amep
ooza upande mmoja si za kweli. blog jumamtanda.blogspot.com ilifanya ziara ya kumteembelea nyumbani kwake Forest mjini Morogoro ili kujua ukweli wa uvumi huo.


Blog ya jamii ya jumamtanda.blogspot.com lilipata taarifa juu ya kuugua kwa  Mahita, ndipo zikafanyika juhudi za kumtafuta na kuzungumza naye nyumbani kwake eneo la Forest kata ya Boma Manispaa ya Morogoro ambapo alishangazwa na uvumi huo na kusema kuwa hiyo ni mara ya pili kwa yeye kuvumishiwa hivyo. 

IGP mstaafu huyo ambaye amestaafu mwaka 2006, akizungumza na mwananshi wa habari hizi nyumba kwake alisema kuwa amekuwa akishangazwa na watu wanaomvumishia kuwa yeye ni mgonjwa na amepooza jambo ambalo si sahihi. 

“Nakumbuka mwaka 2006 nilivumishiwa kuwa naumwa sana, jambo la kushangaza mimi nilikuwa Arusha kikazi kwenye mambo ya TANAPA nikawa napigiwa simu ya kupewa pole nashangaa, sasa hii ni mara ya pili nimepigiwa sana simu za kupewa pole, sijui nani anavumisha hivyi,” alisema Mahita. 

Akizungumzia maisha yake ya sasa Mahita alisema kuwa kwa sasa ajishughulisha na  kilimo katika eneo la Dakawa wilayani Mvomero na amekuwa akilima mazao ya Mpunga, Mahindi na Alizeti.

Alipoulizwa juu ya kuwa na wazo la kugombea nafasi yeyote katika vyama vya siasa aliendelea kukana kuwa hana mpango wa kugombea nafasi yeyote, na kama uvumi huo unatokana na hisia hizo hao wanaofanya hivyo wajipotezea muda.

“Ndugu mwandishi hapa unapoona najiandaa kwenda zangu shambani kupeleka vifaa vya kilimo kwa vijana wangu, kama kuna mtu anafikiria kuwa mimi nataka nafasi yeyote sina mpango huo, najishugulisha na kilimo tu,”alisema IGP huyo mstaafu wa polisi. CHANZO jumamtanda.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: