Nahodha wa klabu ya Darts ya Frendz ya jijini Dar es Salaam, Hemendra Katakia akifurahia kombe baada ya klabu yake kutwaa katika mashindano ya klabu bingwa Tanzania yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa kuifunga klabu ya Ulug
uru ya Morogoro kwa pointi 9-4. JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Na Juma Mtanda, Morogoro.
KLABU ya mchezo wa Dartd ya Uluguru mkoa wa Morogoro imekubali kipigo kikali kutoka kwa klabu ya Frendz ya jijini Dar es Salaam katika mashindano ya klabu bingwa ya taifa kwa kufungwa kwa pointi 9-4 katika mchezo mkali wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa DDC mkoani hapa.
Friendz ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa taifa kufuatia kuilaza klabu ya Rose Garden kwa alama 9-5 huku Uluguru yenyewe ikiilaza Polisi Barracks kwa ushindi wa 9-4 katika michezo yao ya nusu fainali katika mashindano yalianza oktoba 12 mwaka huu.
Kutokana na ubingwa huo Friendz walikabidhiwa kombe, cheti na fedha taslimu kiasi cha sh 500,000 wakati washindi wa pili klabu ya Uluguru ikijipatia zawadi ya Kombe, cheti na fedha sh400,000.
Bingwa wa mashindano hayo atawakilisha nchi katika mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa darts katika ukanda wa Afrika Mashariki ambao mashindano hayo yatakayofanyika mwezi wan ne katika ardhi ya nchi Kenya.
Katika mashindano hayo pia yalishirikisha michezo ya wanawake ambapo klabu ya Kimanga ya jijini Dar es Salaam nayo iliibuka na ubingwa wa taifa kwa upande wa wanawake kufuatia kuilaza klabu ya Polisi kutoka jijini Mbeya huku kwa mchezaji mmoja mmoja, Irene Kihupi kutoka klabu ya Kimanga naye akitawazwa kuwa bingwa wa taifa kumfunga mchezaji hatari wa klabu ya Moro Queens, Fabiola Namajojo kwa pointi 5-4 katika mchezo wa fainali.
Kwa upande wa wachezaji wawili wawili,Wambura Msila na Pastor kutoka timu ya Uluguru walifanikiwa kunyakua ubingwa huo kufuatia kuwabwaga, Gabriel Komba na Adelade Chikoma wa klabu ya Polisi Barracks kwa pointi 4-1 na kujinyakulia zawadi y ash 200,0000.
Mchezaji wa Polisi Barracks, Adelade Chikoma alitwaa ubingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kufuatia kumkung’uta mpinzani wake, John Mlay kutoka klabu ya Kimanga kwa pointi 5-2 na kuambulia zawadi ya sh200,000 na medali.
Mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa vishale mwaka huu yalishirikisha mikoa sita ambayo ni Kilimanjaro,Dodoma, Morogoro,Arusha, Dar es Salaam na Mbeya huku mashindano hayo yakishirikisha klabu 11 za wanaume na wanawake sita.
0 comments:
Post a Comment