BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MARUBANI WAGENI WAVAMIA SOKO LA AJIRA TANZANIA.

Takwimu za TCAA zinaonyesha karibu asilimia 50 ya marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi Tanzania ni wa kigeni. PICHA | MAKTABA.

DAR ES SALAAM. 
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesema ajira ya marubani wazalendo ipo mashak
ani kwa sababu ndege nyingi nchini, zinaongozwa na wageni.
TCAA imesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa na kampuni zinazotoa huduma hizo nchini, kutumia ndege nyingi za kukodi zinazofanya kazi chini ya masharti yanayotoa nafasi kubwa ya kuongozwa na marubani wa kigeni.
“Ndege ni ghali sana na wengi walioko kwenye sekta hii wanakopeshwa na kupewa masharti,”alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhili Manongi, alipokuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti hili.
Alisema karibu asilimia 50 ya marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi hapa nchini, ni wa kigeni.
Manongi alisema ingawa mikataba kuwabana, kigezo cha uzoefu pia ni kikwazo kwa marubani wengi wazalendo.
“Wengine wanashindwa kupata ajira kutokana na kutokuwa na saa zinazohitajika ili mtu aweze kurusha ndege za biashara,” alisema.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa sasa Tanzania ina marubani 500 na katika miaka mitatu ijayo watafikia 700.
Alisema kwa jumla sekta ya usafiri wa anga ina upungufu wa wataalamu kama wahandisi na marubani lakini shida kubwa inawahusu zaidi marubani.
Manongi alisema kwa kuzingatia hali hiyo, TCAA ipo kwenye mikakati ya kuboresha sekta ya marubaini nchini ili pamoja na  mafunzo, pia wapate uzoefu utakaowawezesha kutoa ushindani kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: