Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu, Clara Mwatuka na Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msola katika Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.PICHA NA EDWIN MJWAHUZI.
DODOMA.
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amek
uwa akikiuka kanuni za Bunge.
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amek
uwa akikiuka kanuni za Bunge.
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani
na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli
zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni
kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo
kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza
kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za
wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika
Makinda.
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge
kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na
Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na
wajumbe wa kamati husika.
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja
kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati
inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa
wakipewa Sh130,000.
“Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha
za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao
(Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?” chanzo hicho
kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk
Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya
kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida
hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha
za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana
na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati
hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua
miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao
wanapewa,” alisema Dk Kashililah.
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati
nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi,
ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada
pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
“Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti,
watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda
kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu
zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi
anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo,” alisema Dk Kashililah.
Kuhusu Serukamba.
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika
amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter
Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
“Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili
lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud
Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo
chini ya kamati yake,” kilisema chanzo hicho. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment