Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza wakati wa uzinduzi wa opereshini ya kuondoa wafugaji kijiji cha Bonye, Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini, Innocent Kalog
eris na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera amezindua
operesheni ya kuondoa wafugaji wavamizi zaidi ya 570 na kueleza kuwa utendaji
mbovu wa baadhi ya viongozi kuanzia ngazi ya tarafa hadi kijiji imechangia kwa
kiasi kikubwa kuruhusu mifugo kuingia katika vijiji vya wilaya ya halmasjauri
ya Morogoro bila kufuata taratibu mkoani hapa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wakati wa
uzinduzi wa operesheni hiyo ya kuondoa wafugaji wavamizi, Bendera alisema kuwa
moja ya sababu ya kujaa kwa wafugaji na mifugo yao kumechangiwa na baadhi ya
watendaji kuanzia ngazi ya tarafa hadi kijiji jambo ambalo limechangiwa kwa kiasi
kikubwa mifugo kuingia katika vijiji vya halmashauri ya wilaya ya
Morogoro.
katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha kijiji cha Bonye kata ya Bwakila Chini
mkoani hapa, Bendera alisema kuwa, kuwa watendaji
hao ndiyo chanzo cha uwingi wa mifugo hali iliyopelekea kuwa na migogoro ya
ardhi baina ya walikuma na wafugaji, uharibifu wa misitu, mashamba ya kilimo na uvamizi
wa pori la akiba la seluos game reserve na kuwa njia mojawapo ni kufanya
operesheni ya kuondoa wafugaji wavamizi katika vijiji vyote vya wilaya hiyo.
“Wilaya ya halmashauri ya Morogoro ina jumla ya
wavamizi 575 ambao tayari wamepewa notisi za kuwataka waondoke, baadhi yao wameondoka na
wengine wamekaidi amri hiyo ya kundoka, sasa serikali imedhamilia kusimamia
kikamilifu zoezi hili la kuwaondoa wafugaji wavamizi katika vijiji vyote na
hifadhi za taifa zote zilizopo ndani ya mkoa wa Morogoro”. Alisema Bendera.
Licha hivyo mkuu huyo wa mkoa msafara wake ilishindwa kuendelea na safari yake baada ya kukwama kufuatia basi lililokuwa mbele yao kukwama katika tope kijiji cha Kilengesi katika barabara kuu ya Mvuha-Kisaki.
Bendera alilazimika kukaa eneo hilo na msafara wake hadi gari la polisi lilipovuta basi hilo na wao kupata nafasi ya kupita eneo hilo adha ambayo ilitokana na mchapuo wa barabara kufuatia barabara iliyokuwa ikitumika kujengwa daraja ambalo limefikia hatua za awali.
Naye Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini, Innocent
Kalogeris amewataka wananchi wa vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Morogoro
kutumia vyema operesheni hiyo kwa kuwafichua wafugaji walioshindwa kutii amri
halali ya kuondoka kwa hiari.
Kalogeris alisema kuwa matukio ya migogoro baina ya
wafugaji na wakulima yamekidhiri na kuwa waathirika wakubwa ni wakulima ambao
wengi wao wamekuwa wakiambulia kupata kipigo na uharibufu mkubwa wa mali zao yakiwemo
mazao aina mbalimbali katika mashamba yao.
0 comments:
Post a Comment