BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MSAFARA WA RAIS JAKAYA KIKWETE WAKWAMA KWA MUDA BAADA YA MSITU WA SAO HILL MUFINDI WATEKETEA KWA MOTO KATIKA KUU YA IRINGA-MBEYA LEO.



Msafara wa rais Jakaya Kikwete ukiwa umesimama kwa muda eneo la msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya kufuatia moto mkubwa kuw

aka katika msitu huo mchana wa leo.



Askari polisi akimamisha msafara wa rais Kikwete kutokana na moto mkubwa kutanda eneo hilo la Changalawe katika msitu wa Taifa wa Sao Hill umbali wa mita mbili kuelekea barabara ya Ikulu ndogo mjini Mafinga

Askari wa FFU wakishuka katika gari lao kwenda kuangalia usalama wa rais Kikwete na kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa yamesimama

hapa askari wakishuka kuingia katika moshi mzito kuangalia usalama wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito ulitanda barabarani



Msafara ukipita eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto huo



Huu ndio moto unaoendelea kuteketeza msitu wa taifa wa Sao Hill Mufindi leo

YAKIWA ni masaa takribani mawili kupita kutoka Rais Jakaya Kikwete kufanya kikao chake cha majumuisho ya ziara yake na viongozi wa mkoa wa Njombe na kuwataka kuchukua hatua katika kuthibiti moto ili kuepusha ukame ,moto mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa wa Sao Hill Mufindi na kupelekea msafara wa Rais kusimama kwa muda kiusalama kutoka na moshi mzito uliotanda barabara kuu ya Iringa Mbeya .

Moto ulio ulioanza kuwaka mida ya saa nane mchana ulizuia kwa muda kama dakika tatu hivi msafara wa Rais Kikwete kufimama katika eneo la Changalawe mjini Mafinga umbali wa mita 2 kufika njiapanda ya kuingia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi na Ikulu ndogo ya wilaya ya Mufindi.

Kutokana na tukio hilo la moto msafara wa rais Kikwete ulisimama na baada ya maofisa usalama kushuka na kutazama usalama zaidi wa msafara huo ndipo walioruhusu msafara huo kuendelea .

Hata hivyo jitihada kubwa zilionekana kufanywa na kikosi cha askari wa JKT Mafinga pamoja na wananchi ambao walikuwa wakizima moto huo .

Huku vyombo vya usafiri yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri kutoka Dar es Salaam kuwenda mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania yakikwama kuendelea na safari kutoka na moto huo kushikakasi na moshi mzito kutanda barabara

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema kuwa uongozi wa mkoa tayari umeagiza mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka waliohusika na uchomaji moto huo ili kuchukulia hatua kali.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukichukua hatua kali kwa wale wote wanaoanzisha moto kichaa kama huo hivyo kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika watasakwa popote walipo. 


Mbali na hilo mkuu huyo amelipongeza jeshi la JTK Mafinga kwa kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na moto huo huku akisema madhara zaidi yatokanayo na moto huo yatatolewa baada ya moto huo kuthibitiwa .chanzo Francis Godwin
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: