BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO ANAPASWA KUZALIWA NDANI YA NDOA !!!.

Mtoto akifurahia jambo.

Na Dk. Tengia Urrio.
KAMA kawaida yetu tunaanza makala hii na kifungua mada ambapo tunawasikia ‘washikaji’ wawili wakijadil

iana juu ya jambo fulani linalohusu afya na kutuachia ujumbe fulani.

‘Mshikaji 1’: 

Kumbe sisi wengine tulio humu barabarani, vijijini, mijini na kwenye madaladala ni hifadhi.

‘Mshikaji 2’: 

Unamaanisha kuwa tunaweza tukawa kivutio cha watalii ?

‘Mshikaji 1’: 

Si hifadhi ya wanyama. Namaanisha hifadhi ya maambukizi yanayosambazwa kwa kufanya tendo la uumbaji (MYKKTU) hasa unapolifanya nje ya madhumuni yake. Tunahifadhi maambukizi haya na kuyasambaza kwa wenzetu tunapofanya nao tendo la uumbaji.

Kwa muda wa wiki 3 nimejaribu kueleza kuwa badala ya kuita kile kitendo cha mwanammke na mwanamume kuweka miili yao pamoja kujamiiana, kufanya mapenzi, kufanya tendo la ndoa, kujuana kimwili na misamiati mingi inayojitahidi kulitaja kwa kulificha ficha kwani kulitaja ni kuvunja maadili; tuliite ni tendo la uumbaji.

Wiki iliyopita nilimalizia kwa kusema:“Tukiliita tendo hili tendo la uumbaji ni njia moja ya kuwaambia wale wanaolifanya kwa madhumuni mengine kuwa hili ni tendo la uumbaji; waachie walio na nia ya uumbaji walifanye; waachie walio kwenye ndoa walifanye.

Msomaji mmoja amechangia kwa kusema tukiliita ni tendo la ndoa hapo vilevile tunasisitiza kuwa tendo hili ni tendo linalopaswa kufanywa tu na wale walio kwenye ndoa.

Msomaji: 

Kwangu mimi naona kuliita ni tendo la ndoa ni sahihi zaidi maana tendo lenyewe ninapaswa kufanyika kwenye ndoa. Kuliita ni tendo la ndoa tunasisitiza kuwa kimaadili linapaswa kufanyika ndani ya ndoa. Kuliita ni tendo la ndoa kunawatenga wale wanaolifanya wakati wao si wanandoa.

Hayo ndiyo makusudio yaliyoandikwa kwenye vitabu vyetu vya dini kuwa linafanywa na wale walio kwenye ndoa tu. Ukisema ni tendo la uumbaji unashindwa kuwatambulisha kwa haraka zaidi wale wanaolifanya nje ya ndoa kuwa wanachokifanya ni ubatili kwao.

Neno uumbaji ni kubwa mno na linaingia mno kwenye shughuli inayomhusu Mungu mwenye kuumba. Binadamu hajaumbwa kwa kufanya tendo la ndoa kwani muumbaji ni Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo.

Daktari: 

Naona hatujapishana sana. Wewe na mimi tunakubaliana kuwa ni tendo linalopaswa kufanyika ndani ya ndoa na si vinginevyo. 

Mimi nataka kuliinua tendo hili zaidi; kulipa hadhi kuwa madhumuni yake ni kushirikiana na Mungu katika hii shughuli ya uumbaji ambapo mwanadamu anachangia mwili (yai na mbegu) na Mungu anachangia roho lakini hata mwanadamu kuchangia mwili; yote ni kwa uwezo wa Mungu.

Tutaendelea kuwasikiliza wasomaji wengine wanasemaje. Mimi naendelea kuliita tendo hili ni tendo la uumbaji na kila anayelifanya alifanye huku akijikumbusha kuwa madhumuni yake ni kushiriki katika kumuumba binadamu na si vinginevyo.

 women love viagra to enjoy healthy life relationship Akipata matatizo huko baadaye baada ya kufanya tendo la uumbaji ajikumbushe kuwa yeye amelifanya kwa madhumuni ambayo si ya kushiriki katika kumuumba binadamu.

Leo basi kwa kusisitiza anayosema huyu msomaji kuwa hili ni tendo la ndoa na linapaswa kufanywa na walio kwenye ndoa tu na ninayosema mimi kuwa hili ni tendo la uumbaji na linapaswa kufanywa na wale walio kwenye ndoa tu; tuanze makala mbili zinazosisitiza kuwa kama ni kupata ujauzito huo ujauzito upatikane ndani ya ndoa na si nje ya ndoa; kama ni kuzaa; zaa ndani ya ndoa na si nje ya ndoa.

Kuhusu malezi ya ‘watoto’ kuna wanyama wa aina tatu: Wanyama wasiolea watoto, yaani mama baada ya kujifungua hujiendea zake na kumwacha mwanae akijitafutia mwenyewe mahitaji yake, wanyama ambao watoto hulelewa na mama bila kumshirikisha baba na wanyama ambao watoto hulelewa na baba na mama.

Mwanadamu ni mmojawapo wa wanyama wachache walio kwenye kundi hili la tatu, yaani baba na mama wanashirikiana katika kulea watoto.

Malezi ya wazazi wawili ndiyo yanayomwezesha mtoto kukua kikamilifu kimwili, kiakili, kielimu, kitabia, kimaadili na kiroho.

Kawaida watoto wanalelewa na wazazi wawili. Kulea mtoto na mzazi mmoja si jambo la kawaida na inamnyima mtoto faida ya malezi ya wazazi wawili ya kupata fursa kamili ya kukua kimwili, kiakili, kielimu, kitabia, kimaadili na kiroho.

Mzazi anayemlea mtoto bila mzazi mwenza anakabiliana na matatizo mengi na mwanae anaweza akadhurika kutokana na kutokuwapo kwa baba au mama yake. Mzazi anapojikuta anamlea mtoto bila mzazi mwenza ni vema ajue kuwa malezi haya yana matatizo yanayomhusu yeye na mtoto ili kama inawezekana ayazuie na kama yakitokea akabiliane nayo.

Kwa kuwa kawaida ya malezi ya watoto ni ya kushirikisha wazazi wawili na kwa kuwa mtoto kulelewa na mzazi mmoja kuna madhara hasa kwake yeye mtoto ni muhimu tuzuie pale tunapoweza kuzuia tunapoona kuwa kuna uwezekano mtoto akazaliwa katika hali ambayo atalelewa na mzazi mmoja.

Kwa kuwa kuna matatizo yanayotokea kwa mama na mtoto kama mama anamlea mtoto bila ushirikiano wa mzazi mwenza ni vema kuzuia hali hii ya mzazi mmoja kumlea mtoto bila mzazi mwenza.

Ni vema kuwatambua wasichana wenye ujauzito na hawajaolewa na kuwashawishi na hata kuwawezesha wazazi hawa wawili walioshiriki kwenye tendo la uumbaji na kusababisha ujauzito waoane ili mtoto azaliwe na wazazi walio kwenye ndoa na azaliwe kwenye familia ili aweze kulelewa na wazazi wawili.

Hapa nitaonesha maongezi kati ya daktari na msichana mmoja ambaye amepata ujauzito kabla ya kuolewa na inavyoonekana mtoto atazaliwa kabla wazazi hawajaoana, yaani mtoto hatazaliwa kwenye familia.

Daktari baada ya ‘kuchati’ naye aliona kulikuwa na umuhimu wa kuwashauri kuwa waoane na baba walioshirikiana kwenye tendo la uumbaji ili mtoto azaliwe kwenye familia na alelewe na wazazi wawili.

Utaona kuwa kuchati na huyu msichana kwa simu hakukusaidia kuwashawishi waolewe kabla ya kujifungua. Njia ya kufanyikisha haya ni kwa wafanyakzi wa ustawi wa jamii kuongea na hawa wasichana na wenza wao ana kwa ana. Msichana huyu alianza kwa kuomba ushauri juu ya tatizo la kiafya.

Msichana 1:  

Mimi ni mfanyabiashara ndogo ndogo. Huu ni ujauzito wangu wa kwanza. Eti ukiwa mjamzito huruhusiwi kulala chali? Mimi nalala tu, kwa kulalia ubavu; najipindua, mara kulia mara kushoto na sasa mbavu zinaniuma kweli kweli.

Daktari: 

Oh! Pole sana. Unajua haya ni matatizo ya kuishi mijini mbali na wazazi wetu. Kama ungekuwa kijijini hili jambo ungemuuliza mama, shangazi au mama mkwe au sivyo? Mama mjamzito anajilalia mlalo anaopendelea kulala, ambao haumpi shida. 

Kulala chali ni sawa kabisa mradi tu kulala hivyo hakukupi matatazo au kujisikia maumivu. Ni vigumu bila shaka kulalia tumbo na si vizuri.

Kwa hiyo unaweza ukalala kwa ubavu wa kulia, ukajipindua ukalala chali, ukajipindua ukalalia ubavu wa kushoto na kadhalika. Wakati wa kujifungua utajifungua umelala chali na wakati wa uchungu wa leba utakuwa ukijipindua hivyo hivyo ukitafuta mkao unaoona haukupi shida sana. 


Leba inapochanganya utajikuta umelala chali moja kwa moja mpaka utakapojifungua. Hivi umeolewa?

Msichana: 

Oh! Sina mama mkwe. Sijaolewa lakini nina mchumba. Mungu akipenda tutaoana.

Daktari: 

Ni vizuri kuoana kabla mtoto hajazaliwa ili mtoto azaliwe na wazazi walio kwenye ndoa, kwenye familia. Si vizuri kuishi pamoja bila ndoa. Mungu hapendi.

Msichana: 

Nashukuru kwa ushauri wako ila sijajua kama tutaoana. Vijana wa siku hizi wanakuambia mtaoana halafu kesho yake unasikia kamuoa mwingine. 

Daktari: 
Tunazungumzia kijana huyu mliyepeana mimba si vijana wengine. Huyo uliye na ujauzito wake ungemkazia uzi mwende kwa wazazi wake na wako, mkubalieni muoane mapema kabla mtoto hajazaliwa ili atakapozaliwa azaliwe na wazazi walio kwenye ndoa.

Kama baba na mama zenu hawapo hapo mnapoishi labda kuna ndugu wengine wa kifamilia au marafiki wanaoweza kukusaidieni mkaoana. Hivi kwa sasa mnaishi pamoja au mnaishi mbalimbali?

Msichana: 

Mchumba wangu ndiyo kamaliza chuo mwaka jana na bado anatafuta kazi. Anadai akishapata kazi ndio tutaweka mambo wazi ila rafiki zake wengi wananijua. Kwa sasa hatuishi pamoja. Tunaishi mbalimbali.

Daktari: 

Basi jitahidini kutayarisha maisha yenu ya pamoja ili muweze kuishi pamoja katika ndoa, muweze kumlea mtoto wenu maana mtoto akilelewa na mzazi mmoja au na wazazi ambao hawapo kwenye ndoa haendelei kikamilifu kiafya, kiakili, kielimu, kidini, kimaadili na kimaisha.
pregnant-black-woman
Wiki ijayo tutamsikiliza msichana mwingine ambaye rafiki yake wa kiume anamshinikiza kuwa ni lazima apate ujauzito kabla hawajaoana.
CHANZO TANZANIA DAIMA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: