Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamisi Juma.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alilazimika kuzima mapinduzi yaliyokuwa yamepangwa kuwang’oa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na makamu wake, Mboni Muhit
a.
Jana Kinana akifungua mkutano wa Baraza Kuu la
jumuiya hiyo, aliweka bayana kuwa mkutano huo haukuwa kwa ajili ya
“kuibomoa UVCCM, bali kuijenga”, kauli ambayo inatajwa kuwa iliwavunja
nguvu wajumbe waliokuwa wamepanga kuanzisha harakati za kuwatoa
madarakani viongozi hao.
Habari zaidi kutoka Dodoma zilisema kauli ya
Kinana iliongeza nguvu harakati za kujinasua za Sadifa ambaye usiku wa
kuamkia jana, alikesha akifanya vikao vya kuwaomba radhi wenyeviti wa
UVCCM wa mikoa na baadaye wajumbe wote wa Baraza Kuu.
“Hatua hiyo nadhani imemsaidia sana maana wenzake
ndani ya umoja huo hawaridhiki na jinsi mambo yanavyokwenda, pamoja na
uongozi wake. Wanaona kama hakidhi standards (viwango) zao,” kilisema
chanzo chetu kutoka ndani ya mkutano huo.
Hii ni mara ya pili kwa Katibu Mkuu huyo kumwokoa
Sadifa, kwani Septemba mwaka huu, alilazimika kuingilia kati mgogoro
ambao uliibuka katika kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo Visiwani
Zanzibar baada ya wajumbe kutaka kumwajibisha kwa madai kwamba alikiuka
kanuni za uteuzi wa wakuu wa idara za UVCCM.
Pamoja na kauli elekezi ya Kinana, Sadifa ambaye
pia ni Mbunge wa Donge, Zanzibar alilazimika kucheza sarakasi
zilizomwezesha kuzima mapinduzi yaliyokuwa yameandaliwa dhidi yake.
Mwenyekiti huyo aliongoza kikao cha Baraza Kuu kwa saa tatu na kukamilisha ajenda zilizokuwa zimepangwa, ikiwa ni pamoja na kuwaidhinisha wakuu wapya wa idara za jumuiya hiyo, kisha aliahirisha mkutano huo mara tu baada ya kuibuliwa kwa hoja ya kutaka kumjadili.
Mwenyekiti huyo aliongoza kikao cha Baraza Kuu kwa saa tatu na kukamilisha ajenda zilizokuwa zimepangwa, ikiwa ni pamoja na kuwaidhinisha wakuu wapya wa idara za jumuiya hiyo, kisha aliahirisha mkutano huo mara tu baada ya kuibuliwa kwa hoja ya kutaka kumjadili.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana jioni
zilisema, Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna ndiye
aliyeibua hoja ya kutaka Sadifa ajadiliwe kutokana na kile alichosema
kuwa kiongozi huyo ameifanya jumuiya hiyo kushindwa kutekeleza wajibu
wake ipasavyo.
“Kama tunataka kusonga mbele katika jumuiya yetu,
lazima tuhakikishe kwamba tunaisafisha nyumba yetu ili tukitoka hapa
wote tuwe tunazungumza lugha moja. Kwa hiyo napendekeza mwenyekiti atoke
nje ili tumjadili,” chanzo chetu kilimnukuu Kajuna.
Habari zaidi zilidai mapendekezo hayo ni kama
yaliungwa mkono na baadhi ya wajumbe, akiwamo Mwenyekiti wa UVCCM wa
Mkoa wa Dodoma, Henry Msunga ambaye alisimama na kusema: “Hiyo ni hoja
ya msingi sana”.
Hata hivyo, wakati wajumbe wengine wengi wakiwa
wameinua mikono yao juu wakitaka kuchangia pendekezo hilo, Sadifa
alisimama na kuanza kuzungumza huku akiomba msamaha kwa upungufu wa
kiuongozi unaojitokeza na katika hali isiyotarajiwa aliahirisha rasmi
mkutano huo.
Kajuna na Msunga kwa nyakati tofauti jana,
walilithibitishia gazeti hili kuwapo kwa matukio hayo, lakini walikataa
kuyazungumzia kwa undani huku wakisema kuwa bado wana fursa katika vikao
vijavyo kwa ajili ya kurekebisha mambo ndani ya jumuiya hiyo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment