OFISA wa kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Shirika la Ujasusi la nchini Uingereza, MI5 ameonya kuwa taarifa za siri zilizowekwa hadharani na Edward Snowden hasa kuhusu nchi hiyo kuhusika na kusikiliza mawasiliano ya watu, huenda zikawa zawadi nzuri kwa magaidi kwani hatua ya kuanika upenuni mbinu hizo zimesababisha magaidi wajichunge zaidi na hivyo kudhoofisha nguvu ya majasusi ya kutambua mipango ya magaidi na kuyashughulikia kabla ya hatari.
Kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters, Mkurugenzi wa MI5, Andrew Parker alikiri kuwa wafanyakazi wa
vitengo vya ulinzi na usalama vya nchi za Marekani na Uingereza
vilitegemea sana mawasiliano ya magaidi ili kutengua mitego kabla ya
hatari lakini kwa sasa, kitengo chao cha kusikiliza mawasiliano, GCHQ,
kimepata pigo kubwa kwa kuwa sasa magaidi wanatumia mbinu nyingine ili
kufanikisha mashambulizi waliyopanga.
CHANZO www.wavuti.com
CHANZO www.wavuti.com
0 comments:
Post a Comment