MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda,
amesema vyombo vya dola vinaendelea kukandamiza vyombo vya habari na
kushindwa kuchukua hatua licha ya kutokea matukio ya mauaji, utekeji na
utesw
aji wa waandishi wa habari.
Kibanda ambaye pia ni mwathirika wa utekeji na uteswaji huo, alitoa kauli hiyo jana wakati TEF walipotembelea mnara wa kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Mkoa wa Iringa, Daud Mwangosi, aliyeuawa kwa kulipuliwa bomu na askari polisi kijijini Nyololo wilayani Mufindi, Septemba 2, mwaka jana.
Alisema lengo la ziara hiyo kwa wahariri ni kuwapa fursa ya kuomboleza tukio hilo ambayo hawakuipata kutokana na kutokuwepo wakati wa mazishi ya Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Mkoa wa Iringa.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) ambayo inazalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba, alisema kuwa kutembelea eneo hilo ni jambo linalotoa ujumbe kwa mamlaka na vyombo vya dola kutambua haki ya uhuru wa habari na kujieleza.
Awali Makamu Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga, alisema Mwangosi aliuawa akimtetea mwandishi mwenzake wa gazeti la Nipashe, Godfrey Mushi, aliyekuwa akipigwa na askari baada ya kutokea vurugu kwenye mkutano wa CHADEMA, walipokuwa wakifungua matawi katika Kijiji cha Nyololo.
“Mwangosi alikuwa anamtetea mwandishi wa Nipashe mara baada ya kuona anapigwa, hivyo alipofika sehemu husika na kuwaambia askari kuwa mnayempiga ni mwandishi, wakamgeukia yeye hadi alipofikwa na mauti kwa njia ya bomu lililolipuliwa hatua chache toka tumboni kwake,” alisema Makunga. TANZANIA DAIMA.

0 comments:
Post a Comment