Nairobi.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameeleza kuwa bila
ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada na Mwalimu Julius Nyerere
asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya Idara ya Uhamiaji ya Kenya
kumn
yima hati hiyo ya kusafiria.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi
mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The
Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika
mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati
hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee
Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa
maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.
Hata hivyo, Mzee Jaramongi
aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah wa
Ghana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.
Odinga alihitaji hati
hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomo yake nchini Ujerumani
baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule
ya Maranda.
Katika kitabu hicho, Odinga alisema hakushangaa kunyimwa hati hiyo.
Katibu
wa baba yake aitwaye Olwande K’Oduol alimpeleka kwa Ofisa Afya wa
Halmashauri ya Jiji la Nairobi, Rading Omolo ambapo alipigwa chanjo ya
homa ya manjano.
“Nilipopata cheti cha chanjo hiyo tulirudi nyumbani
kwa K’Oduol ambapo nilikuta vijana wengine wawili Mirulo na Oudia ambao
nao walikuwa wakisafiri nje kusoma, hivyo tukaungana katika safari
moja,” alisema Odinga katika kitabu hicho.
Alisema siku iliyofuatia
waliamka mapema ili wawahi basi la kwenda Dar es Salaam ambapo walifika
kituoni saa 12 asubuhi na waliondoka Nairobi saa 1:30 asubuhi kwa
kutumia basi la kampuni ya Overseas Transport Company (OTC).
Wakati
huo, barabara ya lami ya Nairobi ilikuwa inaishia njiapanda ya Uwanja wa
Ndege wa Jomo Kenyatta na kuanzia hapo hadi Namanga barabara ilikuwa ni
mbaya, anaeeleza Odinga.
“Utaratibu wa kuvuka mpaka ulikuwa rahisi,
tulipata kifungua kinywa katika eneo hilo na kuondoka baada ya muda
ambapo kituo kingine kilikuwa ni Arusha. Basi hilo lilipakia abiria
wengine kabla ya kufika Moshi na kupata chakula cha mchana,” anasema
Odinga na kuongeza.
“Tulipitia Korogwe, Handeni hadi Morogoro ambapo
barabara ya lami ilianza kuonekana tena na tulifika Dar es Salaam saa
1:30 asubuhi baada ya safari ya saa 24 na tulipokelewa na Dola Osman
ambaye alikuwa ni Katibu wa Katibu Mkuu wa TANU, Oscar Kambona.”
Odinga
anaeleza katika kitabu hicho kuwa Osman aliwapeleka hotelini na
kuwaacha kwa kuwa walikuwa wachafu na wenye njaa kutokana na safari
ndefu. Walioga na kubadilisha nguo kisha kupata kifungua kinywa, ndipo
Osman aliporudi na kuchukua picha tatu ndogo kwa kila mmoja ambazo
walitakiwa kuwa nazo.
“Haikuchukua muda mrefu kwani kabla hata
hatujamaliza chakula cha mchana, Osman alirudi na hati zetu za kusafiria
akitueleza kuwa kila kitu kimeshakamilika.
“Siku moja kabla ya
kuondoka kwetu, Osman alituchukua saa 3 asubuhi na kutupeleka ofisini
kwa Waziri Mkuu, Mwalimu Julius Nyerere ambapo Mwalimu alifurahi sana
kutuona na kunieleza kuwa Jaramongi ni rafiki yake wa karibu, pia
alitueleza kuhusu safari yake ya Kisumu mwaka uliopita alipohudhuria
mkutano wa Pan African,” anasema.
Baada ya hayo waliingia kwenye gari
la Nyerere hadi nyumbani kwake ambapo walipata chakula cha mchana,
kisha Mwalimu aliwatakia safari njema na masomo mema. MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA KENYA AELEZA NAMNA MWL JULIUS NYERERE ALIVYOMSAIDIA HADI KWENDA KUSOMA NCHINI UJERUMANI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment