BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK KIKWETE NA MKEWE MAMA SALMA WAWASIRI SALAMA NCHINI SRI LANKA KWA AJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA MADOLA.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Rehabilitation and Reforms wa Sri Lanka Bwana Chandrasiri Gajadeera, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike huko Colombo, mji mkuu wan chi hiyo tarehe 14.11.2013. Mama Salma amefuatana na Rais Kikwete kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike, mjini Colombo Sri Lanka na Mheshimiwa Chandrasiri Gajadeera, Waziri wa Rehabilitation and Reforms wan chi hiyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola unaoanza tarehe 15.11.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiambatana na Mkewe Mama Salma akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bandaranaike nchini Sri Lanka kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola tarehe 14.11.2013.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: