BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAWA NDIYO WAINGEREZA WANAOSAKA REKODI YA DUNIA KWA KUZUNGUKA KWA KUTUMIA USAFIRI WA PIKIPIKI AINA YA BAJAJ, TAYARI NCHI 37 WAMETEMBEA IKIWEMO TANZANIA.

bajaji 10 

Hapa kwenye vumbi, wameandika ni Magharibi mwa Tanzania.
Bajaji 1 

Watanzania wengi tunafahamu Bajaji ni usafiri wa hapa na pale tu, yani sio usafiri wa kubeba abiria kwenye masafa marefu lakini Walimu wawili raia wa Uingereza wamekipiga kibajaji gia na kupita nacho nchi mbalimbali duniani zinazofikia 37.


Ni safari ambayo wameianza August 13 mwaka jana (2012) lakini haijafikia hapa bila matatizo, wanakwambia Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya nchi na kuna wakati injini ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka wakati mwingine wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.


Unaambiwa hii rekodi itaingia kwenye kitabu cha Guiness kama watamaliza safari yao ambayo wamepanga kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha kurudi zao nyumbani Uingereza.


Wanasema wengine wameshindwa kuamini kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a Bajaji ambapo kwenye mpaka wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi ambae aliwaambia haamini kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli, itakua ngumu wao kupata watoto wa kiume.. labda wa kike.
bajaj 3 

bajaj 10 

Wakiwa South Africa.
bajaji 4 

Wakiwa Paris.
bajaji 5 

Wakielekea kwenye mpaka wa Hispania.
bajaji 6 

Barcelona Hispania.
bajaji 7 

bajaji 8 

Wakizungumza na Wanafunzi Ethiopia.
bajaji 9 

Hapa kwenye picha ya juu ni Burundi.
bajaji 11
Ni safari ambayo haijakwenda bila kasoro, hapa ni Northern Peru.
HII NDIO VIDEO BAADHI YA MATUKIO YAO.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: