November 5 2013 ndio stori zilianza kusambaa baada ya ripoti ya
Mbunge wa viti maalum Easter Bulaya bungeni iliyohusu biashara ya dawa
za kulevya huku ikitaja idadi ya Watanzania waliofungwa nchi za nje kwa
kujihusisha na biashara hiyo pamoja na baadhi ya wanaohusika ndani ya
nchi.Baada ya ripoti hiyo, Easter anakiri usiku huo alipata msg nyingi za watu kuhofia maisha yake na nyingine zikimpa pongezi kwa ujasiri alioufanya, ujasiri ambao pia Marehemu Amina Chifupa aliwahi kuufanya.
Kwenye taarifa mpya aliyoitoa kwa millardayo.com Easter Bulaya amekiri kupokea vitisho vya maisha kutoka kwa watu asiowafahamu kitu kilichofanya aanze kubadili hata jinsi ya kuishi.
‘Namshukuru Mungu kwamba niko hai na nimefurahi kupigiwa simu na Wachungaji na Sheikh wakiniombea baada ya kuiona ripoti yangu ila simu za kutishiwa maisha nimepigiwa mara mbili na private number… mwanzo ilikua msg za pongezi tu na kuhofia maisha yangu kwa ujasiri nilioufanya ila sasa ni vitisho mpaka nyumbani kwangu’ – Easter.
Kwenye sentensi hii, Easter anasema ‘tulimaliza bunge Jumamosi vitisho vya simu vikaanza Jumanne vikidai vitanikomesha, naamini mtu kama siku zimefika huwezi kukimbia kivuli chako kama wameamua kukufanyia la kukufanyia watakufanyia tu…
kuna siku mtu alikuja nyumbani kwangu akagonga saa tano usiku nikamuuliza wewe nani ili nikufungulie akakataa kutaja jina lake na kusema wewe njoo nifungulie nina shida na wewe, nikamwambia sikufungulii ndio akaniambia we kataa lakini tutakupata tu’.

0 comments:
Post a Comment