BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUPOROMOKA KWA JENGO NA KUAWAWA ZAIDI YA WATU 50 KWAMFANYA WAZIRI MKUU WA LATVIA KUACHIA NGAZI CHEO HICHO.

http://kresy24.pl/wp-content/uploads/2013/06/dombrovskis_valdis_waldis_dombrowskis.jpgWAZIRI Mkuu wa wa Latvia, Valdis Dombrovskis, amejiuzulu kufuatia kuporomoka kwa jengo moja nchini humo, Alhamisi iliyopita na kusababisha watu wapatao hamsini kuuawa.



Bwana Dombrovskis amesema amekubali kuwajibika kisiasa kutokana na mkasa huo ambapo paa ya duka moja kubwa la bidhaa katika mji mkuu, Riga, lilipinda na kuporomoka.


Polisi wameanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini kama taratibu za ujenzi wa jengo hilo zilizingatiwa au la; bustani ilikuwa ikijengwa juu ya paa la jengo hilo la maduka wakati ajali hiyo ikitokea.


Latvia imekuwa na siku tatu za maombolezo kuwakumbuka waathirika wa janga hilo, ambalo ni baya kuwahi kutokea nchini Latvia, tangu nchi hiyo ijipatie uhuru wake mwaka 1981.


Kujiuzulu kwa Bwana Dombrovskis, ambaye ameiongoza Latvia katika kipindi cha mgogoro wa kiuchumi, kumekuja wiki kadhaa kabla ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: