Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na mwenzake wa Marekani Johh Kerry mjini Geneva.
MAAFISA wa Israel wameshtumu vikali mkataba wa nuklia na Iran
uliofikiwa mapema Jumapili mjini Geneva. Wanasema mkataba huo kamwe
huzuii Iran kuendelea na juhudi zake za kutengeneza silaha za nuklia.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alishtumu vikali mkataba wa
nuklia wa Iran mara tu ulipotangazwa akisema “ huu sio mkataba wa
kihistoria, ni kosa la kihistoria.”
Netanyahu alisema dunia inakabiliwa na hatari zaidi kutokana na kile
alichoita utawala hatari zaidi duniani ambao umepiga hatua kubwa
katika azma yake ya kupata silaha hatari duniani.
Bw. Netanyahu aliongeza kuwa Israel ina wajibu wa kujilinda kutokana na
vitisho vyovyote vile na akaapa kuwa hatakubalia Iran kutengeneza silaha
za nuklia.
Iran pamoja na nchi sita sita zenye nguvu duniani zilitangaza kufikiwa
mkataba huo wa muda Jumapili alfajiri baada ya siku nne za majadiliano
mazito.
Mkataba huo unailazimu Iran kukubalia wakaguzi wa kimataifa wa silaha za
nuklia kukagua viwanda vyake vya nuklia kwa maelewano kuwa ikiwa itatii
masharti yote yaliyowekwa,haitawekewa vikwazo vya kiuchumi kwa miezi
sita.
Lakini Israel na baadhi ya serikali za Magharibi zinasema zitafanya
maamuzi zenyewe juu ya kutumia majeshi kushambulia viwanda vyovyote vile
vya nuklia nchini Iran endapo zitagundua kuwa vipo.http://www.voaswahili.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MAAFISA WA ISRAEL WANUNA KISA MAKUBALIANO YA YALIYOFIKIWA NA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI JUU YA MKTABA WA NUKLIA NA NCHI YA IRAN.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment