BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAPIGANO YA MAJESHI YA SERIKALI YA DRC CONGO NA KUNDI LA WAASI LA M23 LASABABISHA VIFO 900, HUKU M23 WAKIPOTEZA WAPIGANAJI WAKE ZAIDI YA 700.

JESHI la DRC Congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei.
Wanajeshi wa Serikali ya DRC wakiwa mjini Goma kujiandaa kukabiliana na waasi wa M23Wanajeshi wa Serikali ya DRC wakiwa mjini Goma kujiandaa kukabiliana na waasi wa M23. RFI


Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700 waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Wanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa kwenye makabiliano hayo.


Pia wapiganaji 72 wa Rwanda na wapiganaji 28 wa Uganda waliuawa.


Mwanzoni mwa mwezi huu, waasi wa M23 walitolewa na jeshi la serikali iliyoungwa mkono na kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 wa Umoja wa Mataifa lakini serikali ya Congo na waasi walikosa kuelewana kuhusu mpango wa baadae wa amani.


Waasi wa M23 walisitisha vita na kujisalimisha baada ya jeshi la DRC kwa ushirikiano na wanajeshi wa UN kupigwa vita vikali na kuwaondosha katika maeneo waliyokuwa wameyateka.


Maelfu ya wakaazi wa Mashariki mwa DRC walilazimia kukimbilia nchi jirani ya Uganda kutafuta hifadhi wakati kundi hilo lilipokuwa linaendesha uasi wao na hata kuuteka mji wa Goma kwa muda.


Kudni la M23 lilifanya vitendo vya kikatili dhidi ya watu wa Mashariki mwa DRC ikiwemo ubakaji na kuwatumia watoto kama wapiganaji. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: