Mchezo wa soka ndiyo mchezo unapendwa zaidi na wapenzi wengi wa michezo mingine duniani na hapa inadhihilisha hilo katika kitongoji cha Gongo kijiji cha Mgata kata ya Bwakilajuu halmashauri ya wilaya ya Morogoro, juu ya kilele cha mlima Mondo unaonekana uwanja wa mchezo wa miguu kwa ajili ya watoto kucheza soka mara baada ya kumaliza shughuli zao hasa zile za masomo ama wikiendi hujazana hapo kusakata kabumbu.
Picha hii ilipigwa Novemba 11 mwaka huu majira ya saa 8 mchana wakati mwandishi wa blog hii akifuatiliwa tukio la mauaji ya kutatanisha ya kikongwe Hellan Petri Mahunzila (75) aliyeuawa kisha mwili wake kutupwa ukiwa umechunwa ngozi kufuatia kutekwa nyakati za usiku oktoba 2/ 2013.
TUKIO hilo la kifo cha kikongwe huyo, Hellan Petri Mahunzila ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku 12 kisha siku ya
13 mwili wake kuonekana kando ya shamba lake huku maiti yake ikiwa imechunwa
ngozi mwili mzima, imezua hofu kubwa na kukubikwa na usiri wa mauaji hayo huku wakazi
wa kitongoji cha Gongo kijiji cha Mgata kata ya Bwakilajuu mkoani Morogoro
wakiishi kama mnyama digidigi ambaye amekuwa akiwindwa na binadamu kwa ajili ya
kitoweo.
MAKALA YA HABARI HIYO INATARAJIWA KUCHAPISHWA KATIKA GAZETI LA MWANANCHI NA MTANDA BLOG HIVI KARIBUNI.
0 comments:
Post a Comment