MBEYA JAMANI KUNA NINI ?. IMANI ZA KISHIRIKINA ZAZIDI KUSUMBUA AKILI ZAO HUKU MZEE PASCAL MWANJALANJE AKINUSURIKA KUZIKWA AKIWA HAI KUTOKANA NA KIFO CHA GHAFLA CHA BINTI MMOJA.
IKIWA zimepita wiki takribani mbili baada ya mwanaume mmoja kuzikwa akiwa hai eneo la kijiji cha Mshewe wilaya ya Mbeya Vijijini mkoan hapa, mwanaume mwingine wa kijiji cha Shilanga wilayani humo, amenusurika kuzikwa akiwa hai jana.
Taarifa kutoka eneo la tukio, zimemtaja mzee aliyenusurika kuzikwa akiwa hai kuwa ni Pascal Mwanjalanje, aliyetuhumiwa katika kifo cha binti mmoja kijijini hapo aliyekufa katika mazingira yanayodhaniwa kuwa ni ya utata.
Wakizungumza na kalulunga blog, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shilanga, wamesema kuwa, kuna binti wa kijiji hicho alikwenda kufua mtoni na baada ya kumaliza aliwaambia wenzake kuwa anataka kupumzika, kisha akajilaza kwenye majani na kifo kikampata akiwa amejilaza.
Kutokana na tukio hilo, vijana wakachimba kaburi na kugomea kuuzika mwili wa mwanamke huyo kwa madai kuwa hakukuwa na mtu aliyekufa hivyo akatafutwa mzee Mwanjalanje anayetuhumiwa kumloga ili azikwe, na baada ya jitihada za kumzika mzee huyo kugonga mwamba walifukia kaburi.na Kalulunga blog
0 comments:
Post a Comment