Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe (kushoto)akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha
na Edwin Mjwahuzi.
DAR ES SALAAM.
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema kuwa hana mpango wa kujiondoa Chadema na kusisitiza kwamba atakuwa mtu wa mwisho kujitoa ndani ya chama hicho kwa hiari yake.
DAR ES SALAAM.
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema kuwa hana mpango wa kujiondoa Chadema na kusisitiza kwamba atakuwa mtu wa mwisho kujitoa ndani ya chama hicho kwa hiari yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana katika mkutano aliouandaa kwa pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati
Kuu, Dk Kitila Mkumbo, Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alisema kwamba
amekuwa mwanachama wa Chadema tangu akiwa na umri wa miaka 16 hivyo
haiyumkiniki akikimbia chama hicho.
Zitto na Dk Kitila walivuliwa nyadhifa zao wiki iliyopita wakihutumiwa kukihujumu chama hicho.
“Kuna watu ambao walitegemea kuwa leo hii
ningejibu mapigo, ‘ningezodoa,’ watu wengine kwa majina kama ilivyo
kawaida kwa siasa za Tanzania. Natambua pia kama ilivyo kawaida wakati
wa migogoro kwa vyama hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo
ningetangaza kinachoitwa ‘maamuzi magumu’,” alisema na kuongeza:
“Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia
nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu,
napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia wote nchini watambue
kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa
mwisho kutoka kwa hiari yangu.”
“Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano
ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya
wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda
siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka.”
Alisema kuwa atafuata taratibu zote za ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hilo.
“Mimi sitoki, wanaotaka nitoke, wanitoe wao,” alisema Zitto.
Zitto alisema Chadema ndicho chama kilichomlea na
kumfikisha hapo alipo sasa, hivyo hata siku moja hatokuwa chanzo cha
kuvunjika kwa chama hicho.
“Ningependa hata mtoto wangu akikua, awe pia
mwanachama wa chama hiki, nimejiunga na chama hiki nikiwa na umri wa
miaka 16 mpaka sasa nina miaka 37, nimetumia muda mrefu zaidi Chadema
kuliko kipindi chote cha maisha yangu, Chadema ni kama maisha yangu,
kukivunja chama hiki ni sawa na kujivunja mimi mwenyewe, kitu ambacho
siwezi,” alisema Zitto. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment