BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMUZI WA BENDI YA FM ACADEMIA APOTEZA MAISHA CHINA KUFUATIA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKU KIFO CHAKE KIKIKUBIKWA NA UTATA.

KUMRADHI KWA MUONEKANO WA PICHA HII.

MWANAMUZIKI aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa.

 


Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo nchini China, rapa huyo alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact, Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu. 



“Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho. 



Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu aliwasiliana na Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot. 



Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa. 



“Haristot alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi. Credit: GPL


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: