BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UFARANSA YAONGEZA MAJESHI ILI KUIMARISHA HALI YA USALAMA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI BAADA YA KUTOKEA HALI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

 
Majeshi ya Ufaransa yakiwa ndani ya Kifaru cha kijeshi

WIZARA ya Ulinzi ya Ufaransa imethibitisha kuwa imetuma mamia ya wanajeshi wa ziada kwenda kusaidia kuimairisha hali ya usalama Jamuhuri ya Afrika ya Kati.



Maafisa ya Umoja wa Mataifa umesema hali ya usalama nchini humo ni ya wasiwasi huku ikionya huenda mauaji ya halaiki yanaweza kuendelea.


Ufaransa imekuwa ikitoa msukumo kwa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa ambalo linazungumzia namna ya kuyasaidia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema raia katika eneo la Jamuhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakikumbana na matatizo yaliyozidi uwezo wao ikiwa ni pamoja na unyanyasi wa kijinsia, utesaji, mauaji na fujo kati ya wakristo na waislamu.


Majeshi ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakijaribu kuimarisha hali ya usalama nchini Afrika ya Kati tangu Rais Francois Bozize apinduliwa mwezi Marchi.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: