DAR ES SALAAM.
HALI ya wasiwasi iligubika eneo kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana.
HALI ya wasiwasi iligubika eneo kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana.
Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard),
uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho
ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo
yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito.
Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na
wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi
ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko
na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu.
Maelekezo ya ulinzi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwasili
ukumbini hapo saa 5.20 asubuhi na baada ya kuingia, wapiga picha
waliruhusiwa kuingia kuchukua kumbukumbu ya tukio hilo kwa dakika moja
tu.
Waandishi wa habari hawakutakiwa kuingia na badala yake walielezwa kuwa wangepewa taarifa baadaye.
Wakati wapiga picha wakiwa ndani, mmoja wa wajumbe
wa mkutano huo alitoka na kutoa maelekezo kwa walinzi wa Chadema
akiwataka kuwa makini kutekeleza kazi yao watakapopewa amri ya kumwondoa
mjumbe yeyote mkutanoni.
“Kama mkipewa amri ya kuondoa mtu ingieni na
mtekeleze amri hiyo mara moja,” alisisitiza mjumbe huyo na kuingia ndani
haraka. Walinzi hao zaidi ya 10, walipokea maelekezo hayo kwa kutikisa
kichwa kuashiria kukubaliana na amri hiyo.
Kikao kufunguliwa
Kikao hicho ambacho kilifunguliwa dakika nane baada ya Mbowe kuwasili, kilipangwa kujadili mambo matatu jana.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema kingepitia taarifa za vikao viwili vya Kamati
Kuu vilivyopita.
Suala jingine ambalo lilipangwa kujadiliwa jana ni
ushiriki wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar na kupitia taarifa ya fedha.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment