BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WA SERIKALI YA RAIS DK JAKAYA MRISHO KIKWETE, UTENDAJI DHAIFU LAKINI WANA KIPATO KIKUBWA.



Mh. Rais Jakaya Kikwete.


DAR ES SALAAM.  
RIPOTI mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.




Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.


Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.


Akizindua ripoti hiyo iliyochunguza gharama za kuwalipa viongozi wa Serikali na wanasiasa, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), Dk Theodore Valentine, alisema kuwa viongozi wa Afrika Mashariki ndio wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa zaidi chini ya Jangwa la Sahara.


“Kama viongozi wakuu watakuwa wanalipwa mishahara mikubwa, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaweza kugharimia demokrasia?” alihoji Valentine.


Utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2012, umebainisha kuwa Rais wa Tanzania analipwa mshahara dola 172,014 kwa mwaka (Sh275 milioni) sawa na Sh22.9 milioni kwa mwezi, huku Rais wa Kenya, akiongoza kwa kulipwa dola 515,021 kwa mwaka (Sh824 milioni) kwa mwaka sawa na Sh68.6 milioni kwa mwezi.


Rais wa Rwanda analipwa dola 199,000 kwa mwaka (Sh124 milioni) sawa na Sh10 milioni kwa mwezi, wakati rais wa Nigeria akipokea dola 161,902 (Sh259 milioni) ambazo ni sawa na Sh21 milioni kwa mwezi.


Pia umeeleza kuwa Rais wa Kenya analipwa mara 320 zaidi ya pato la mwananchi wa kawaida wa nchi hiyo, wakati rais wa Afrika Kusini anapata mara 46 na Rwanda mara 150 zaidi ya mwananchi wa kawaida.


Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kuwa rais wa Tanzania analipwa mara 8.2 ya mshahara wa hakimu, huku rais wa Kenya akipokea mara 13.1 na kumpita rais wa Rwanda anayechukua mara 12 zaidi ya mshahara wa hakimu.


Kwa upande wa wabunge, utafiti huo umeeleza kuwa wabunge wa Tanzania wanalipwa mara 3.0 ya mshahara anaolipwa hakimu, Kenya (5.5) na Rwanda (3.0). Viwango hivyo vimetajwa kuwa vikubwa kuliko vya wabunge wa Nigeria na Afrika Kusini.


Naibu Spika anena

Naye Naibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai alisema kuwa umefika wakati ambapo mishahara ya viongozi wa umma inabidi iwekwe wazi kwa wananchi. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: