BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKATI SERIKALI IKISISITIZA HUDUMA YA DAMU HOSPITALINI NI BURE, BAADHI YA MADAKTARI NA WAUGUZI WAMEGUZA DILI NA KUWAUZIA WAGONJWA HAPA NCHINI.

Damu salama ikiwa imehifadhiwa kwenye mfuko maalumu wa kutunzi damu. Picha na Maktaba.
 
DAR ES SALAAM NA MIKOANI
WAKATI Serikali ikisisitiza kuwa huduma ya kumwongezea mgonjwa damu hospitalini ni bure, imebainika kwamba baadhi ya watu mitaani wakiwamo wabeba mizigo sokoni wanauza damu zao kwa watu wanaohitaji.



Mbali ya watu kuuza damu zao, majimaji hayo mekundu muhimu mwilini yamegeuka bidhaa adimu baada ya baadhi ya wauguzi na madaktari nao kugeuza huduma hiyo kuwa kitegauchumi chao.


Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ni kosa kwa mtumishi yeyote wa afya nchini kumuuzia mgonjwa damu na wala hakuna biashara ya kuuza damu kwa kuwa hutolewa bure na watu wanachangia kwa hiari.


Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili katika hospitali mbalimbali nchini, umebaini hospitali nyingi hazina damu za kutosha na hivyo kusababisha baadhi ya wagonjwa kuwalipa watu mitaani, ili kuwatolea damu au kuinunua kwa wauguzi na madakari.


Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema kuwa wahudumu wa afya wanaoendesha vitendo hivyo ni watu wanaojaribu kuizidi maarifa Serikali na kwamba wananchi wamepewa taarifa za kutosha kuwa damu haiuzwi.


“Kuna watu wanajaribu kutuzidi maarifa, hiyo ni tabia inayopaswa kupigwa vita. Mtu yeyote atakayetakiwa kununua damu, atoe taarifa kwa mganga mkuu au kituo chochote cha polisi,” alisema.


Mkoani Dodoma

Wabeba mizigo wa soko la Majengo Mjini Dodoma, wamekuwa mkombozi kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali ya mkoa huo baada ya kugeuza miili yao kuwa sehemu ya kuvuna damu na kuiuza kwa ndugu wa wagonjwa hao.


Gharama za kuuza damu hiyo ni kati ya Sh10,000 hadi Sh30,000 kwa chupa moja, kutegemea na uwezo wa ndugu wa mgonjwa huyo, lakini baadhi wamekuwa wakitoa zaidi kama sehemu ya shukurani.


Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuthibitishwa na baadhi ya wabeba mizigo hao, imebainika kuwa kitendo cha kutoa damu kwa wabeba mizigo ni cha kawaida na kwamba utaratibu huo ulianza muda mrefu.


Enock Ayub ambaye ni mmoja wa watu ambao wamechangia damu zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti, alilimbia gazeti hili kuwa biashara ya kutoa damu anaipenda na kwamba inampa matumaini ya kuishi kwa kuamini kuwa bado ni mzima.


“Mimi nimechangia damu zaidi ya mara tatu, lakini tukifika kule tunabadilisha majina maana madaktari wanataka mtu ukae muda za miezi sita bila ya kutoa, sisi tunataka fedha ‘mkwanja’, hatuna jinsi,” alisema Ayubu na kuongeza. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: