MATUKIO YA KISIASA.
Majaji katika mahakama ya ICC.
WANACHAMA wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wamerekebisha baadhi
ya sheria za Mkataba wa mahakama hiyo hapo jana kutoa nafasi kwa
washtakiwa kufuatilia kesi zao kupitia vidio.
Mahakama hiyo iliyo na wanachama 122 ilifikia uamuzi huo katika mkutano wake wa kila mwaka, uliofanyika katika makao yake makuu, mjini The Hague, Uholanzi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto.
Katika siku za nyuma, majaji wa mahakama ya ICC waliwahi kumuachia Naibu Rais William Ruto, anayeshitakiwa kwa kesi sawa na Rais Kenyatta, ya kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi, aendelee kuwepo nchini Kenya kwa baadhi ya kesi zake ili aweze kutimiza wajibu wake serikalini.
Marekani yaridhia mabadiliko
Mabadiliko yaliofanywa hapo jana yanaweza kuwa na maana kwa kwa washitakiwa waliojitolea kushirikiana na mahakama hiyo kama Uhuru na Ruto kuliko wale walioshikiliwa kwa nguvu na kuwekwa rumande.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power.
Samantha Power, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema uamuzi huo umewekwa katika hali ya kwamba unalinda haki ya washtakiwa na waathiriwa, huku ukitoa nafasi ya kesi hiyo kuendelea bila kupoteza wakati.
Rais Uhuru Kenyatta, makamu wake Wiiliam Ruto na mtangazaji wa Radio Moja nchini humo Joshua Arap Sang wote wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC.
Kenya yataka viongozi wanaoshtakiwa kupewa msamaha
Kenya imekuwa ikijihusisha na mipango ya kidiplomasia ya kusimamisha kwa muda kesi ya Uhuru na Ruto huku ikisema kuwa nchi hiyo na eneo la Afrika ya Mashariki kwa jumla linahitaji uongozi thabiti katika kupambana na wanamgambo wa al-Shabaab katika nchi jirani ya Somalia.
Kundi hilo la Al shabaab linalosemekana kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaida.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Kenya Amina Mohammed.
Thuluthi mbili ya wanachma 122 wa mahakama ya ICC wanapaswa kupigia kura uamuzi kama huo wa kubadilisha Mkataba wa Rome ulioiunda Mahakama hiyo na utaingia katika utekelezwaji mwaka mmoja baada ya sehemu kubwa ya nchi wanachama kuuridhia.
Hata hivyo katika hali nyengine iliojitokeza ni kwamba balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Macharia Kamau amesema wanachokitaka wao sio kutumika kwa mfumo wa video katika kesi ila kuondoa kabisa mashtaka kwa viongozi walioko madarakani. DW

0 comments:
Post a Comment