Michelle akiteta jambo na Helle.
WASHINGTON, Marekani.
NDOA ya Rais Barak Obama na mkewe Michelle haitaweza kuvunjika kwa sasa kwa vile mke huyo mrembo atatakiwa kuendelea kuishi katika Ikulu ya White House hadi mumewe atakapomaliza muhula wake wa pili wa uongozi mwaka 2016.
Obama
akiwa 'busy' na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati
wa mazishi ya Mandela Afrika Kusini. Kulia ni mkewe Michelle.
Obama
akimbusu Helle Thorning-Schmidt mbele ya mkewe. Kwa mujibu wa vyanzo
mbalimbali, Michelle, mama wa watoto wawili, Sasha na Malia, hata kama
ataachika atalazimika kuendelea kubakia ikulu kwa ajili ya mahitaji ya
kuwa pamoja na mumewe katika hafla za kiserikali zinazohitaji uwepo wa
mke. Hiyo ndiyo sera ya Ikulu ya Marekani.
Akifurahia jambo wakati mkewe kanuna.
Juzi, Gazeti la The Nation la Marekani liliripoti kuparaganyika kwa ndoa hiyo iliyowahi kutajwa kama ndiyo bora zaidi duniani, kwa kile kilichoelezwa kuwa kuchukia kwa Michelle baada ya kumwona mumewe akishoboka na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt wakati wa shughuli za kumuaga rais wa zamani wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela ‘Madiba’.
Obama
akipiga picha na Helle. Vyanzo katika mitandao mbalimbali vilisema ndoa
hiyo ilikuwa inawaka moto kwa muda mrefu na kwamba hata kabla Michelle
hajaanza kuishi katika jengo la peke yake katika viwanja hivyo vya
ikulu, walikuwa wakilala ‘mzungu wa nne’.
Helle akimuonyesha kitu Obama. Mwaka 2012, uvumi ulisambaa kwa kasi duniani ukielezea kutengana kwa watu hao wawili maarufu zaidi, hali iliyosababisha Ikulu ya Marekani kukanusha taarifa hizo.
Michelle baada ya kuamua kukaa kati yao. Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na ikulu, Obama wala Michelle juu ya madai ya kutengana kwao.

0 comments:
Post a Comment