TASWIRA YA MSAFARI WA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA ABDULRAHMAN KINANA KUTOKA MAKAMBAKO KUELEKEA DAR ES SALAAM NDIYO HUO.
Treni ikipita katika 'tanuru' ndani ya mlima wakati ikitoka Makambako kwenda Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30, Desemba 9, 2013, kwa teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kwenye behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), kukagua stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro, wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30, Desemba 9, 2013, kwa teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakishuka kwenye treni katika stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mlimba wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Selemani Balali (kulia) aliposhuka na msafara wake, kwenye stesheni ya Mlimba, akiwa njiani kutoka Makambako kwenda Dar es Salaam, jana
Kinana na msafara wake, wakiwa na viongozi wa Kata ya Mlimba, alipokwenda kukagua stesheni ya eneo hilo. Mbele ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
Kinana, Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye wakitoka kukagua jengo la stesheni ya Mlimba(P.T)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua karanga kwa mwananchi aliyekuwa akifanya biashara ya karanga hizo kwemye stesheni ya Mlimba, Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro
Kinana akimlipa fedha muuzaji huyo wa karanga, Josephine Amani
Kinana akiuliza bei ya embe zilizkuwa zinauzwa na mwananchi kwenye stesheni ya Mlimba
Kinana na Nape wakiuliza bei ya samaki kwa muuzaji wa bidhaa hiyo kwenye stesheni ya Mlimba, jana
Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakitazama samaki waliokuwa wanauzwa kwenye stesheni ya Mlimba
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga stori na baadhi ya wasafiri kwenye stesheni ya Mlimba.
Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na mmoja wa viongozi wa CCM waliompokea Kinana na msafara wake kwenye stesheni ya Mlimba
Abiria akipitisha mtoto dirishani wakati treni inatoka Makambako
Treni ikichana msitu kwenda Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment