BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIKOSI VYA JESHI VYAFANIKIWA KUTIBUA MAPINDUZI SUDAN KUSINI

59D9A9A4-69A8-4F4C-8E86-9FF0663BC5F3_mw1024_n_s_f229c.jpg
RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.


Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer.


Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo.
Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.


Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: