Maandamano mjini Kiev.
UPINZANI nchini Ukraine unamatumaini kuwa waandamanaji hadi alfu kumi watajitokeza leo Jumapili na kutoa msukumo mpya kudai kwa Rais Viktor Yanukovich ajiuzulu kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.
Vyama vikuu vitatu vya upinzani vimesema vinaanzisha , "kikosi cha taifa
cha upinzani" baada ya polisi wa kuziwia ghasia kuwatawanya waandamanji
kwa kutumia nguvu na kuwajeruhi watu kadha jana Jumamosi.UPINZANI nchini Ukraine unamatumaini kuwa waandamanaji hadi alfu kumi watajitokeza leo Jumapili na kutoa msukumo mpya kudai kwa Rais Viktor Yanukovich ajiuzulu kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.
Mkutano huo wa waungaji mkono upinzani ulivunjwa na polisi waliotumia virungu ambao waliwashambulia kiasi ya waandamanaji 1,000 katika uwanja wa uhuru katika mji mkuu Kiev mapema jana Jumamosi asubuhi (30.11.2013).
Maandamano zaidi
Upinzani umetoa wito wa kufanyika maandamano mapya leo katikati ya mji wa Kiev baada ya polisi kuzingira uwanja huo wa uhuru kwa kuweka uzio wa chuma.
"Tunaweza na tunapaswa kuwaondoa viongozi hawa," bingwa wa dunia wa ngumi Vitali Klitschko , kiongozi wa chama cha UDAR amewaambia waungaji mkono upinzani wapatao 10,000 siku ya jumamosi, na kutangaza maandamano mapya.
Vitali Klitschko kiongozi wa chama cha UDAR.
Umoja wa Ulaya umeishutumu Urusi kwa kuipa mbinyo Ukraine, nchi ambayo inategemea kwa kiasi kikubwa gesi kutoka Urusi, na kujitoa kutoka katika makubaliano hayo.
Matumizi ya nguvu na vitisho
Jana Jumamosi , Lithuania ambayo inashikilia uongozi wa Umoja wa Ulaya kwa sasa imesema matumizi ya nguvu "hayavumiliki" na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja huo Catherine Ashton pamoja na kamishna wa upanuzi wa Umoja huo Stefan Fuele wametoa wito wa kufanyika uchunguzi.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU, Catherine Ashton
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa maafisa nchini Ukraine kutimiza wajibu wao wa kulinda haki za binadamu.
Jana Jumamosi, Yanukovich alisema katika taarifa kuwa, "amefadhaishwa mno" na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na ameapa kuwa waliohusika wataadhibiwa.W.
0 comments:
Post a Comment