BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HABARI MPYA !!! DK KITILA NA MWIGAMBA WAVULIWA UANACHAMA NDANI YA CHAMA CHA CHADEMA


Dk.Kitila Mkumbo aliyetimuliwa uanachama Chadema.

KAMATI Kuu ya Chadema iliyokutana Januari 3-4, 2014 katika Ukumbi wa Mbezi Garden, jijini Dar es Salaam imeamua kuwavua uanachama Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kuanzia jana.Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.
Akizungumza na wanahabari leo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa amesema malengo ya waraka wa mabadiliko waliokutwa nao wahusika hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa viongozi wa chama.
Ameongeza kuwa, chama kinawatangazia wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na washirika wake kwa jina la Chadema.
Samson Mwigamba ambaye naye amevuliwa uanachama wa Chadema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: