BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CHADEMA NUSURA ZILIPULIWE NA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kulikuwa na jaribio la kutaka kuzichoma moto ofisi zake za makao makuu zilizopo baada ya watu wasiojulikana kufika usiku wa manane na kulilipua moto gari mojawapo la chama hicho.
Gari lililotaka kuchomwa moto na watu hao ambao waliwasha moto tanki la mafuta ni lenye namba za usajiri T 588 AAJ aina ya Fuso ambalo limekuwa likitumiwa na chama hicho kwenye operesheni zake mikoani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, alisema jalada la uchunguzi wa suala hilo limeshafunguliwa na walinzi wa ofisi hizo wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.


Wambura alisema hata hivyo, gari hilo halikupata madhara makubwa na kwamba suala hili lisitafsiriwe kwamba kulikuwa na njama za kutaka kuzichoma moto ofisi za Chadema.


“Hatujui kama kulikuwa na jaribio la kutaka kuzichoma ofisi za Chadema, kilichopo pale ni gari lao ambalo inadawa lilitaka kuchomwa moto hivyo tafsiri ya kwamba ofisi za chama zilitaka kuchomwa moto sijui linatoka wapi,” alisema.


Awali Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare (pichani), alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana saa 8:00.


Alisema tayari chama hicho kimeripoti taarifa hizo katika kituo cha polisi kidogo cha Kinondoni na kufunguliwa jalada la upelelezi namba KMJ/RB/133/14 .


Lwakatare alisema walinzi wa ofisi hizo waliona gari ambalo lilikuwa limefichwa namba na watu wawili waliteremka na mmoja kuelekea usawa wa nyumba ya kulala wageni inayotazamana na ofisi za Chadema.


Alisema walinzi hawakuwatilia mashaka watu hao kwa sababu walifahamu ni wageni ambao walikuwa wamefikia katika nyumba hiyo ya kulala wageni.


Dakika tano baadaye baada ya watu hao kuondoka, walinzi wa ofisi hiyo walishangaa kuona moshi ukifuka kutoka chini ya gari hilo na kuomba msaada kwa majirani ambao waliamka na kuanza kuzima moto kwa kutumia mchanga na maji na hivyo kulinusuru gari hilo kupata athari zaidi. SOURCE: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: